Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
9 8 /
U O N G O F U & W I T O
wengine. Daima kumbuka kwamba mwalimu wako yuko wazi na tayari kutembea pamoja na wewe katika hili. Uwe na uhakika, pia, kwamba viongozi wa kanisa lako (hasa mchungaji wako) wanaweza kuwa na namna maalum ya kukusaidia kujibu maswali yoyote magumu yanayotokana na kutafakari kwako juu ya somo hili. Kuwa wazi kwa Mungu na umruhusu akuongoze jinsi anavyotaka. Mwombe Mungu alithibitishe Neno lake kwa ishara na maajabu katika maisha yako, na katika maisha ya wale unaowahudumia. Dai ahadi mahususi ya Mungu katika Isaya 55:8 11, kwamba Neno la Mungu haliwezi kurudi bure au tupu, bali litatimiza kusudi alilolituma.
MAZOEZI
Warumi 10:8-13
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/books kupata kazi ya usomaji ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.
Kazi ya Usomaji
3
Kama kawaida unapaswa kuja na ripoti yako ya mgao wa usomaji iliyo na muhtasari wako wa maeneo ya kusoma kwa wiki husika. Pia, ni muhimu sasa uwe umechagua andiko kwa ajili ya kazi yako ya ufafanuzi wa Maandiko, na uwasilishe mapendekezo yako kuhusu kazi yako ya huduma kwa vitendo. Katika somo letu la mwisho tutalitazama Neno takatifu la Mungu kama Neno Linaloita. Tutajifunza jinsi Neno linavyotuita kwenye ufuasi, kuziishi ajabu za hadithi yake katika mfumo wa maisha ya kujitoa kwa dhati katika ufuasi. Tunaagizwa kujitoa kwa Yesu bila masharti ili tuweze kumpenda zaidi, tukichukua utambulisho wa wageni na wasafiri katika ulimwengu huu, kama watumwa kwa utukufu wake. Kama watumwa wake katika ulimwengu huu, vile tuliyo na yote tuliyo nayo katika maisha haya yanapaswa kutolewa wakfu katika kumjua Mungu na kumfanya ajulikane. Zaidi ya hayo, tutachunguza jinsi Neno la Mungu linavyotuita kuishi na kufanya kazi katika jamii, kuishi tukiwa huru katika Kristo kama fursa ya upendo na uinjilisti, na utume; kutimiza Agizo Kuu, kufanya vita na adui yetu wa kiroho Ibilisi, na kuakisi maisha ya Ufalme kupitia upendo na matendo yetu mema.
Kazi Nyingine
ukurasa 197 15
Kuelekea Somo Linalofuata
Made with FlippingBook flipbook maker