Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 9 7

U O N G O F U & W I T O

Kwa nje, Neno huleta utambulisho na ushirika pamoja na watu wa Mungu, udhihirisho wa tabia na mtindo mpya wa maisha yanayomfanania Kristo, upendo kwa waamini wengine, na shauku ya kuona waliopotea wakivutwa kwa Kristo.

Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo yaliyojadiliwa katika somo hili kuhusu uwezo wa Neno la Mungu kubadilisha na kugeuza, unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Henrichsen, Walt. Layman’s Guide to Applying the Bible . Grand Rapids: Zondervan Books, 1985. Kuhatschek, Jack. Applying the Bible . Grand Rapids: Zondervan Books, 1990. Lewis. C. S. Mere Christianity . New York: Macmillan Company, 1960. Stott, J. R. W. Understanding the Bible . Glendale: Regal Books, 1972. Kiini cha mafunzo haya ni kutafuta kuhusianisha kweli hizi na huduma yako kupitia kanisa lako. Katika kufikiria juu ya nguvu ya kugeuza ya Neno la Mungu, ni changamoto gani mahususi, masuala, au hali gani unazokabiliana nazo sasa katika huduma ambapo ni lazima kweli hizi zitumike na kueleweka? Katika masuala yote yanayohusiana na huduma ya mijini, pengine hakuna lililo kubwa kama suala hili muhimu: ujasiri wetu na uwezo wetu katika kulihudumia Neno la Mungu, na uwezo wa Neno katika kugeuza na kubadilisha maisha ya wale tunaowahudumia. Zingatia fursa mbalimbali za huduma unazoshiriki, na umwombe Roho Mtakatifu akufundishe ni maeneo gani na jinsi gani unaweza kuwa na uwezo wa kufikiria upya hali au masuala yanayoendelea kwa kuzingatia mafundisho ya somo hili la Neno la Mungu. Unapofikiria kuhusu kazi yako ya huduma kwa vitendo kwa ajili ya moduli hii, unaweza kuitumia ili kupanua ufahamu wako juu ya kweli hizi kwa namna ya kivitendo zaidi. Utafute uso wa Mungu kwa ajili ya kupokea ufahamu zaidi, na urudi wiki ijayo tayari kuwashirikisha wanafunzi wenzako maarifa utakayoyapata. Bila shaka unajua mifano na hali mahususi sasa hivi ambapo wewe au wale unaowahudumia wanahitaji kushuhudia nguvu ya Neno la Mungu ya kugeuza na kubadilisha maisha. Huenda baadhi ya mahitaji na hali hizo zimefafanuliwa zaidi kupitia kujifunza kwako Neno la Mungu, na uwezo wake wa kugeuza na kubadilisha. Usisite kutafuta mtu wa kushirikiana naye katika maombi ambaye anaweza kushiriki kuubeba mzigo wako na kuinua maombi haya mahususi kwa ajili ya nguvu ya Neno iwezayo kuleta mageuzi katika maisha yako na maisha ya

Nyenzo na Bibliografia

Kuhusianisha Somo na Huduma

3

Ushauri na Maombi

ukurasa 196  14

Made with FlippingBook flipbook maker