Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
9 6 /
U O N G O F U & W I T O
Itachukua Muda Gani?
Hivi majuzi, vijana watatu waliongozwa katika sala ili kumpokea Kristo ndani ya bustani fulani ambapo kundi la vijana wahuni wa mtaa huo hukutana. Kundi hili kimahususi limejikita sana katika maoni na tabia za ubaguzi wa rangi dhidi ya jamii zinazochukuliwa kama jamii duni, lakini vijana hao ni wabaya zaidi linapokuja suala la maoni yao kuhusu watu Weusi na Wahispania. Zaidi ya wiki tatu zilizopita, kumeshuhudiwa mabadiliko ya kweli katika maisha ya vijana hawa ambao wamekuwa wakija kanisani na kushiriki ibada za vikundi vidogo (ushemasi). Hata hivyo, kila mara inaonekana kwamba bado kuna mabaki ya ubaguzi wa rangi katika tabia zao. Baadhi ya watu katika kusanyiko wana mashaka juu ya wokovu wa vijana hao, huku wengine wakiwatetea kwamba Mungu anafanya kazi katika maisha yao na ataendelea kufanya kazi hiyo kadri wanavyoendelea kukua katika Kristo. Ni aina gani ya mabadiliko tunaweza kutarajia katika maisha ya vijana hawa, na ikiwa inachukua muda kushinda, itachukua muda gani kwao kuondokana na utumwa wao wa zamani kuhusiana na suala la ubaguzi wa rangi? Katika kikundi kidogo cha uanafunzi wa Biblia kwa washirika wapya, dada mpendwa fulani anapata shida sana kila wiki kuhusu suala la kuomba hadharani. Yeye ni mwenye aibu, na anapenda kuomba peke yake, lakini ana tatizo la kweli kabisa la kuomba kwa sauti, mbele ya wengine. Hana uhakika, hata hivyo, ikiwa kuomba kwa sauti ni muhimu. “Je, Yesu hakutuambia twende chumbani na kuomba faraghani? Kwa nini basi ni muhimu sana kusali pamoja na wengine kwa sauti kubwa?” Je, ni ushauri gani hasa ungempa dada huyu ili kumsaidia kuelewa kwamba kuomba ni mojawapo ya ishara za uongofu tunazopaswa kutarajia kutoka kwa watu wote waliookoka kweli? Je! ni muhimu kwake kujifunza jinsi ya kufanya hivyo hadharani? Iwapo ataendelea kukataa kuomba hadharani, je, hilo linaonyesha kwamba huenda hajaokoka? Ikiwa ndiyo au hapana, kwa nini? Injili ya Yesu Kristo ni Neno linalogeuza. Roho wa Mungu anatumia Neno kuzalisha metanoia , yaani, toba ya dhambi na kumgeukia Mungu katika Yesu Kristo. Kazi hii pia huzalisha imani ( pistis ), ambayo humwokoa na kumkomboa mwamini na adhabu, nguvu, na uwepo wa dhambi. Neno la Mungu, mara linapoamilishwa na toba na imani, huzalisha ishara zinazothibitisha msamaha wa Mungu na uwepo wa nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. Kwa ndani, ishara hizo zinajumuisha ujuzi wa Mungu kama Baba wa mbinguni, uzoefu mpya wa maombi, uwazi kwa Neno la Mungu, na nia ya kufuata uongozi wa ndani wa sauti ya Yesu. “Sijisikii Amani Kufanya Hivyo.”
3
3
4
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook flipbook maker