Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 9 5
U O N G O F U & W I T O
* Je, Neno laMungu linabadilisha kwa ufanisi jinsi gani mtazamo na matendo ya mtu aliyeamini? Je, ni muhimu kwetu kujua hasa jinsi mchakato huu unavyofanya kazi moyoni? Ikiwa ndiyo au hapana, kwa nini? * Kwa nini wakati fulani inaonekana kana kwamba Neno la Mungu halina matokeo yoyote katika maisha na mtazamo wa watu, hata waamini? Tatizo ni nini ikiwa Neno linafundishwa na bado hakuna kitu kinachoonekana kutokea katika maisha ya mtu yeyote kama matokeo? * Je, tunapaswa kutazamia aina fulani ya mabadiliko au mwitikio kutokea kila wakati tunapotoa Neno la Mungu kwa wengine, iwe wale wanaosikia Neno hilo ni waamini au la? Elezea jibu lako. Kikundi cha Mafunzo ya Biblia kanisani kilipojifunza Injili ya Luka pamoja, mjadala mkali ulitokea miongoni mwa washiriki juu ya asili ya toba. Wengine walianza kubishana kwamba kwa kuwa tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani pekee, ni makosa kusema kwamba toba ni tofauti na imani. Walitoa hoja yao kwamba wakati wowote mtu anapogeuka na kumwamini Yesu, toba ni sehemu ya imani hiyo. Wengine walisema kwamba toba ni tendo tofauti ambalo linakuja kabla ya imani. Wengine walizidi kuchanganyikiwa kadri muda ulivyoendelea, wakiwa hawaelewi kabisa swali hilo, au hata umuhimu wa mada yenyewe. Ikiwa ungepewa jukumu la kuwasaidia kuelewa hoja husika, ungewafundisha nini na ungefanya nini hasa? Kuna mhudumu mpya wa vijana ambaye amekuja kanisani kwenu na Mungu anaonekana kumtumia kwa kiwango kikubwa sana. Watoto zaidi na zaidi wanakuja kwenye matukio ya huduma ya vijana, na wengi wa vijana wanaikiri imani kupitia matamasha mbalimbali ya ibada na mikutano ya injili inayoandaliwa na kanisa. Kwa kuwa idadi imeongezeka, wengine wameanza kujiuliza ikiwa watoto wengi wanakuja kwa ajili ya madhumuni mengine tofauti na kumfuata Bwana. Wengi wa watoto hao wanaendelea kuvaa kama zamani, wengi wanaendelea kuvuta sigara, na hata kutukana, wakati wengine wanaonekana kuwa wamebadilika kabisa. Je, unaweza kujadiliana nini na mtumishi huyu wa vijana juu ya masuala ya mabadiliko na uongofu, ikiwa atakuuliza maoni yako kuhusu kinachoendelea? Je, Toba Yafaa Kueleweka kama “Kazi”? Ikiwa Hakuna Ishara, Hakuna Wokovu
MIFANO
1
3
ukurasa 196 13
2
Made with FlippingBook flipbook maker