Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

9 4 /

U O N G O F U & W I T O

³ Neno hili ambalo hufanya kazi kwa ufanisi kuleta toba ( metanoia) kwa ajili ya wokovu, hufanya kazi kwa nguvu ileile kuzalisha imani ( pistis ) ndani ya mtu. Imani katika Neno la Mungu ndiyo njia ambayo Baba humwokoa na kumkomboa mtu na adhabu, nguvu, na uwepo wa dhambi. ³ Kama matokeo ya toba na imani katika Neno la Mungu, ishara mpya za msamaha wa Mungu na nguvu za Roho Mtakatifu zinadhihirishwa ndani ya moyo wa mwamini na kupitia maisha yake. ³ Maisha ya ndani ya mwamini hubadilishwa na Neno la Mungu. Kwa ndani, mwamini huhisi na kupata uzoefu wa ishara za maisha mapya katika Yesu Kristo, zikijumuisha ujuzi wa Mungu kama Baba wa mbinguni, uzoefu mpya wa maombi, uwazi kwa Neno la Mungu, na nia ya kufuata uongozi wa ndani wa sauti ya Yesu. ³ Neno la Mungu lina nguvu na lina uwezo katika kutoa pia ishara za nje, halisi za maisha mapya ndani ya Mkristo. Hizi ni pamoja na vitu kama vile kujitambulisha na kuwa na ushirika na watu wa Mungu, udhihirisho wa tabia na mtindo mpya wa maisha yanayomfanania Kristo, upendo kwa waamini wengine, na shauku ya kuona waliopotea wakivutwa kwa Kristo. ³ Sola gratia (kwa neema pekee) na sola fides (kwa njia ya imani pekee) ni maneno ya Kilatini yenye manufaa ambayo yanatoa muhtasari wa asili ya uongofu kupitia imani katika Injili ya Yesu Kristo. Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani pekee, yaani, kwa kutegemea kazi ya Yesu Kristo msalabani. Neema hii na imani hii pekee ndiyo msingi wa ukombozi na msamaha wa Mungu. Sasa ni wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu asili ya nguvu ya kugeuza ya Neno la Mungu. Fikiria kwa umakini kuhusu mawazo yako kwa habari ya uongofu kupitia toba na imani, na uyaangazie haya sasa katika mjadala wako. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia yale ambayo umejifunza hivi punde? Labda baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, mtu anaweza kudai kuwa anamjua Mungu kwa ukaribu na haonyeshi ishara za ndani au za nje za kuokoka? Kwa nini ni muhimu kwa yule anayedai kumjua Mungu kuonyesha ishara fulani ya uongofu wa kweli katika maisha yake?

3

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi

Made with FlippingBook flipbook maker