Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 9 3

U O N G O F U & W I T O

2. Maandiko yanaelezeaje uzoefu wa maombi kama ishara ya kugeuzwa na Neno la Mungu? 3. Kama matokeo ya ushawishi wa Neno la Mungu katika moyo wa mwamini, ni aina gani ya mtazamo na matendo yatatokea kuhusiana na shauku yake ya kulielewa Neno la Mungu na kufuata amri za Yesu? 4. Je, ni lazima mtu aonyeshe ishara zozote kati ya hizi (au nyinginezo) za uongofu ili kudai kwamba yeye ni wa Mungu? Je, inawezekana kuokoka na kutoonyesha dalili za mabadiliko ya ndani? Ikiwa ndiyo au hapana, kwa nini? 5. Ni upi mtazamo wa kila mwamini wa kweli kuhusiana na watu wa Mungu, Kanisa? Je, inawezekana kudumisha uhusiano wa karibu sana na Mungu katika Kristo na kutojali Wakristo wengine? Ikiwa ndiyo au hapana, kwa nini? 6. Kuna uhusiano gani kati ya kumpenda Yesu na kuwapenda waamini wengine? Elezea. 7. Neno la Mungu linapoleta uongofu, hubadilisha mtazamo wa mwamini kuhusu waliopotea. Eleza jinsi Neno la Mungu linavyobadilisha uhusiano wa mwamini mpya na wale wasiomjua Yesu. 8. Je, kweli mtu anaweza kudai kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yesu ikiwa haonyeshi kuwa na shauku ya kuona wengine wakimjia na kumjua Kristo? Elezea jibu lako. Somo hili linalenga katika uwezo wa Neno la Mungu wa kuumba maisha mapya ndani ya mwamini kwa njia ya toba na imani, kumkomboa mwamini kutoka katika athari na nguvu ya dhambi, na kuzalisha ndani ya moyo na maisha ishara mpya muhimu za uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu. Neno linageuza, yaani, linabadilisha maisha ya waamini, likiwavuta kwa Mungu, kwa njia ya Kristo, na kuwapa shauku ya kumtukuza Mungu katika nyanja zote na nyakati zote za maisha yao. ³ Neno linalogeuza kwa lugha nyingine ni habari njema ya wokovu kwa imani katika Yesu Kristo. Injili ya Yesu Kristo ndilo Neno linalogeuza. ³ Neno la Mungu humwongoza mwamini kwenye metanoia , yaani, kutubu dhambi na kumgeukia Mungu kwa njia ya Yesu Kristo kwa kuiamini Injili.

3

MUUNGANIKO

Muhtasari wa Dhana Muhimu

ukurasa 196  12

Made with FlippingBook flipbook maker