Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

9 2 /

U O N G O F U & W I T O

2. Tutaimimina mioyo yetu katika maombi kwa ajili ya waliopotea , Rum. 10:1.

3. Tutazidi kuwa tayari kutoa dhabihu kubwa kwa niaba ya wale waliopotea, ili wapate kumjua Bwana, Rum. 9:1-3.

Hitimisho

» Neno Lile Linalogeuza ni Neno hai lenye nguvu linalozaa ishara za maisha mapya, za ndani na za nje katika maisha ya Mkristo aliyeiamini kweli. » Neno hilo lililo hai hutokeza uthibitisho mwingi ndani ya moyo wa Mkristo kwamba yeye ni mali ya Mungu, ukijumuisha ujuzi wa hakika wa Mungu kama Baba yake, uzoefu mpya wa maombi na ushirika na Mungu, uwazi na njaa ya Neno la Mungu kama lishe, na utayari wa kufuata uongozi wa ndani wa sauti ya Yesu kama Mchungaji wake. » Neno hilo pia hutoa ishara za nje za nguvu ya Neno iletayo badiliko. Miongoni mwa mambo mengine, linazalisha ushirika wa hadhara na utambulisho pamoja na watu wa Mungu, udhihirisho wa shauku mpya, maadili na mtindo wa maisha kupitia tabia mpya inayomfanania Kristo, upendo kwa waamini wengine, na kiu inayoongezeka ya kuona waliopotea wakirudi kwa Yesu Kristo. Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kupitia kile ulichojifunza katika sehemu ya pili ya video. Msingi wa tumaini na nguvu zetu katika huduma ni uwezo na nguvu ya Neno la Mungu kuzaa ndani ya mwamini matunda halisi. Tunasonga mbele katika kushirikisha Neno la Mungu kwa sababu ya imani kamili tuliyo nayo katika uwezo wa Maandiko wa kubadilisha maisha ya wale wanaolikubali na kuliamini. Tafadhali jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Ni kwa njia gani Neno la Mungu linabadilisha uhusiano wa mwamini mpya na Baba? Je, mwamini mpya atakuwa na uhakika wa aina gani kuhusu uhusiano wake mpya na Mungu kupitia imani katika Kristo na uwepo wa Roho ndani yake?

3

Sehemu ya 2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

ukurasa 195  11

Made with FlippingBook flipbook maker