Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 3 Wito wa Utakatifu Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Utakatifu
Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.
~ 1 Wathesalonike 4:7
Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;
~ Waefeso 4:1
Ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.
~ 1 Wathesalonike 2:12
Uongozi wa kiroho unahitaji watu waliojazwa na Roho. Sifa nyingine ni muhimu; lakini kujazwa na Roho ni jambo la lazima. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni hadithi ya watu walioanzisha Kanisa na kuongoza shughuli ya kimishenari. Ni jambo la muhimu kiasi kikubwa mno kwamba sifa kuu ya wale ambao walitakiwa kuchukua hata nyadhifa za chini za madaraka katika Kanisa la kwanza ilikuwa kwamba wawe watu “waliojaa Roho Mtakatifu.” Maafisa hawa walipaswa kujulikana kwa uadilifu na uwezo wa kufanya maamuzi, lakini hasa kwa hali yao ya kiroho. Mtu anaweza kuwa na akili nzuri na kuwa na ustadi wa kiutawala. Lakini bila kuwa mtu wa rohoni ( sic ) hana uwezo wa kutekeleza uongozi halisi wa kiroho. Nyuma ya shughuli zote za mitume kulikuwa na utendaji mkuu wa Roho. Kama msimamizi mkuu wa Kanisa na mwanamkakati mkuu wa shughuli za kimishenari anajulikana kila mahali. . . . Uteuzi wa viongozi wa Ufalme haupaswi kuongozwa na hekima ya ulimwengu, mali, au hadhi. Jambo kuu la kuzingatia ni hali ya kiroho. Kanisa au shirika la kimisheni linapofuata seti tofauti ya vigezo, kimsingi huko ni kumwondoa Roho kutoka kwenye uongozi.
~ J. Oswald Sanders. Spiritual Leadership . 2nd Edition. Chicago: Moody Press, 1994. uk. 79-80.
33
Made with FlippingBook Digital Publishing Software