Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

This is the Swahili edition of the Foundations for Ministry course "An Authentic Calling".

M F U LU L I ZO WA K OZ I ZA M I N I G I YA H UDUMA

Utume katika Miji

W ITO H ALISI : K UMWAKILISHA K RISTO NA U FALME WAKE KUPITIA K ANISA

Dk. Don L. Davis

The Urban Ministry Institute, ni Huduma ya World Impact, Inc.

SWAHILI

M FULUL I ZO WA K OZ I ZA M I S INGI YA H UDUMA

Utume katika Miji

U2-401

W ITO H ALISI : K UMWAKILISHA K RISTO NA U FALME W AKE K UPITIA K ANISA

Dkt. Don L. Davis

The Urban Ministry Institute, ni Huduma ya World Impact, Inc.

© 2010, 2012. The Urban Ministry Institute. Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya:

T he Urban Ministry Institute 3701 East 13th St. North, Suite 100 Wichita, KS 67208

© 2025 Kiswahili

Kimetafsiriwa na: Sam Gripper Mhariri: Eresh Tchakubuta

ISBN: 978-1-62932-432-6

Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.

Yaliyomo

Kuhusu Mwandishi

5

Dibaji

7

11 Kipindi cha 1 Utangulizi Kutambua Eneo Lako la Huduma katika Jumuiya ya Kiagano ya Mungu

23 Kipindi cha 2

Wito wa Wokovu Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Wokovu

33 Kipindi cha 3

Wito wa Utakatifu Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Utakatifu

45 Kipindi cha 4

Wito wa Uhuru Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Uhuru

57 Kipindi cha 5

Wito kwa Jumuiya Kuelewa Wito Halisi kama Wito kwa Jumuiya

69 Kipindi cha 6

Wito wa Utumishi Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Utumishi

81 Kipindi cha 7

Wito wa Mateso Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Mateso

Viambatisho

93

Bibliografia

167

Kuhusu Mwandishi

Mch. Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi wa Urban Ministry Institute. Alipata Shahada ya Sanaa (B.A.) katika Masomo ya Biblia kutoka chuo cha Wheaton, Shahada ya Umahiri (M.A.) katika Theolojia ya Utaratibu kutoka shule ya Uzamili ya Wheaton, na ana Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Theolojia na Maadili kutoka Chuo Kikuu cha lowa Kitivo cha Dini. Dkt. Davis amefundisha kama profesa wa dini na theolojia kwenye vyuo na seminari kadhaa, ikiwemo chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha Mt. Ambrose, na Chuo cha Shahada za Juu za Theolojia cha Houston. Tangu mwaka 1975, ametumika na World Impact, ambayo ni shirika la kimisheni lisilofungamana na dhehebu moja, na lililojikita katika uinjilisti, ufuasi, na upandaji wa makanisa mijini katika miji ya Marekani. Don ni mzungumzaji wa mara kwa mara katika makongamano na mikutano ya kitaifa, na anatumika pia kama Makamu wa Raisi wa Maendeleo ya Uongozi wa World Impact. Ni mhadhiri wa Staley na mwanachama wa American Academy of Religion. Kwa miaka mingi Dkt. Davis ameandika mitaala, kozi na nyenzo nyingi zilizotengenezwa ili kuwaandaa wachungaji, wapanda makanisa, na watenda kazi wa kikristo kwa ajili ya huduma bora na yenye ufanisi katika mazingira ya mijini, ikiwemo Mtaala wa Capstone, ambao ni mtaala wa The Urban Ministry Institute wa ngazi ya seminari wenye moduli kumi na sita uliotengenezwa maalum kwa ajili ya kuwaendeleza viongozi wa makanisa ya mjini.

5

Dibaji

The Urban Ministry Institute ni kituo cha utafiti na maendeleo ya uongozi cha World Impact, shirika la umisheni wa Kikristo lisilofungamana na dhehebu moja lililojikita katika uinjilisti na upandaji wa makanisa katika miji ya Marekani. Taasisi ya (TUMI) iliyoanzishwa Wichita, Kansas mwaka wa 1995, imefadhili kozi, warsha, na matukio ya mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa mijini ndani ya nchi tangu mwaka 1996. Kwa miaka mingi tumerekodi na kufanyia mapitio sehemu kubwa ya nyenzo hizi, na sasa tunazifanya zipatikane kwa wengine ambao wanawaandaa viongozi kwa ajili ya Kanisa la mjini. Mfululizo wa kozi zetu za Misingi ya Huduma unawakilisha sehemu kubwa ya mafunzo yetu ya ana kwa ana yanayotolewa kwa wanafunzi wa ndani hapa Wichita. Tunashukuru na kufurahi kwamba sasa nyenzo hizi zinaweza kupatikana kwako. Tuna uhakika kwamba utaweza kukua sana unapojifunza Neno la Mungu na kuuhusisha ujumbe wake wa haki na neema kwenye maisha na huduma yako. Kwa faida yako binafsi, tumejumuisha nyenzo zetu za kawaida za darasani pamoja na rekodi zake za sauti kwa kila kipindi cha darasa, zikiwa zimewekwa katika mfumo utakao kuwezesha kujisomea mwenyewe. Tumeacha nafasi ya ziada katika nyenzo halisi zilizochapishwa ili uweze kuongeza vidokezo na maoni wakati unaposikiliza rekodi husika. Hili litakusaidia sana unapochunguza zaidi mawazo na mada hizi. Kumbuka, mafunzo katika vipindi hivi yalitolewa katika mazingira ya darasani na kwa njia ya warsha katika Chuo chetu cha Huduma cha Hope School of Ministry. Hii inamaanisha kwamba, ingawa vitabu vilitengenezwa kwa ajili ya wanafunzi ili waweze kufuatilia na kuhusika na zile rekodi kwa karibu, panaweza kuwepo na tofauti kadhaa. Kwa hiyo, unaposhughulika na nyenzo hizi, tafadhali kumbuka kwamba namba za kurasa katika rekodi haziendani na namba za kurasa katika kitabu. Ombi letu la dhati ni kwamba kozi hii ya Mfululizo wa Kozi za Misingi ya Huduma itathibitika kuwa ya baraka na yenye kukutia moyo katika mwenendo na huduma yako kwa Kristo. Kwa hiyo, Bwana na aitumie kozi hii kuongeza uelewa wako wa Neno lake, ili kwamba ujazwe maarifa na kuandaliwa kutimiza kazi aliyonayo kwa ajili yako katika huduma ya Ufalme.

7

8 Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Kusudi kuu la somo hili ni kuchunguza kwa pamoja kile ambacho Maandiko yanafundisha juu ya vipengele na majukumu yanayohusiana na wito wa Mungu kwa Kanisa na uongozi wake. Zaidi ya hayo, tutachunguza kwa karibu inamaanisha nini mtu kutimiza wito wake maalum kwa kumwakilisha Yesu Kristo na Ufalme wake kwa heshima na uadilifu kupitia Kanisa. Kama matokeo ya kuchukua kozi hii, kila mwanafunzi anapaswa kuwa na uwezo wa: • Kunukuu, kufafanua, na kutumia kwa ufanisi maandiko teule yanayotoa muhtasari na kuelezea vipengele na majukumu yanayohusiana na wito halisi wa Mungu. • Kutofautisha kati ya dhana ya wito wa jumla na wito maalum wa Mungu kwa ajili ya uongozi katika Kanisa. • Kukariri na kuelezea asili ya wito wa Mungu unaohusiana na wokovu, utakatifu, uhuru na jumuiya. • Kutoa Maandiko na hoja za kuelezea wajibu wa pande mbili wa utumishi na mateso yanayohusiana na wito wa Mungu. • Kutoa muhtasari kuhusu hatua za kuelewa na kuthibitisha wito maalum wa Mungu. • Kujadili na kutoa ushahidi wa wito wako binafsi kwenye huduma, na kueleza kile unachoamini sasa kuwa ndio wito wa Mungu kwenye maisha yako, iwe katika Kanisa au katika jukumu fulani la uongozi katika Kanisa kama mwakilishi rasmi. • Kukariri kifungu teuliwa cha Maandiko kuhusu wito wa Mungu. Jambo la muhimu zaidi katika ufuasi na huduma ni mtu kutambua wito wake katika Yesu Kristo. Kama Bwana, yeye peke yake ndiye anayejiitia wanaume na wanawake, wavulana na wasichana kutoka kila nchi, tamaduni na koo ili watengwe kwa ajili yake na ufalme wake, ili watumike kama watumwa na wafungwa kwa ajili ya utukufu wake na kwa faida ya Injili. Mtu kutoa yote kwa Kristo ni kupokea yote yatokayo kwake wakati huo huo, na kwa wito huo, uzima wa milele. Bwana na akupe neema na masikio ya kusikia sauti yake ya ufasaha, na wito wake wa ujasiri na mwaliko kwa maisha ya ufuasi, huduma, na kumshuhudia Yeye na Ufalme wake.

~ Don Davis

Dibaji

9

Kazi na Usahihishaji Kwa vituo vyetu vya TUMI, nyenzo zote zinazohusiana na kozi hii ziko katika www.tumi.org/foundations. Kila kozi au warsha imeainishiwa vitabu vya kiada ambavyo vinapaswa kusomwa na kujadiliwa katika kipindi chote cha kozi. Tumeweka orodha yetu rasmi ya vitabu vya kiada vya Mfululizo wa Kozi za Misingi ya Huduma katika www.tumi.org/foundationsbooks .

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia foundations@tumi.org.

Kipinidi cha 1 Utangulizi Kutambua Eneo lako la Utumishi katika Jumuiya ya Kiagano ya Mungu

Viongozi wa kweli ni wachache. Watu na vikundi huwatafuta kila wakati. Katika Biblia yote, Mungu anatafuta viongozi pia. “Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake” (1 Sam. 13:14). “Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.” (Yer. 5:1). “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka” (Eze. 22:30). Biblia inatuonyesha kwamba Mungu anapompata mtu aliye tayari kuongoza, kujitoa katika ufuasi kamili na kuchukua jukumu kwa ajili ya wengine, mtu huyo anatumiwa kwa viwango vya juu. Viongozi wa aina hii bado huwa na mapungufu na kasoro, lakini pamoja na hayo, wanafanyika viongozi wa kiroho. Hivyo ndivyo walivyokuwa watu kama Musa, Gideoni, na Daudi. Na katika historia ya Kanisa, Martin Luther, John Wesley, Adoniram Judson, William Carey, na wengine wengi [ wakiwemo Debora, Esta, Mariamu, na katika Kanisa Sojourner Truth, Elisabeth Elliott, Mama Theresa, na Aimee Semple McPherson , italiki ni yangu]. Kuwa kiongozi katika Kanisa daima kumekuwa kukihitaji nguvu na imani izidiyo ile ya mwanadamu wa kawaida. Kwa nini hitaji letu la viongozi ni kubwa, na viongozi waliopo ni wachache mno? Kila kizazi kinakabiliwa na mahitaji makubwa ya uongozi wa kiroho, na huwapata wachache wanaojitokeza kuhudumu.

~ J. Oswald Sanders. Spiritual Leadership . Toleo la 2. Chicago: Moody Press, 1994. uk. 18.

I. Theolojia Simulizi na Hadithi ya Kutoka: Kutafuta Mbinu Inayoaminika ya Kitheolojia ili Kuelewa Wito wa Mungu.

Musa na Wito wa Mungu Kut. 3:1-10 – Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. 3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. 4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. 5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana

11

12

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu. 6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. 7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; 8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. 10 Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”

2 Kor. 4:6 Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Gal. 1:15-17 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, 16 alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; 17 wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski.

A. Wito wa kinabii wa Mungu: Mchungaji wa kondoo mwenye umri wa miaka 80, mwali wa moto katika kichaka kinachowaka, na shauku ya Mungu ya kuokoa watu kwa ajili yake mwenyewe (Kut. 3:2-10).

1. Ishara ya kujifunua: mwali wa moto kutoka kwenye kichaka, Kut. 3:2

2. Maelezo na maelekezo ya BWANA, Kut. 3:4

3. Mwitikio wa aliyeitwa, Kut. 3:4

4. Utambulisho wa Mungu kwa aliyeitwa, Kut. 3:5-6

5. Agizo la Mungu, Kut. 3:7-10

Kumbuka: muundo huu unarudiwa katika miito mingi ya kinabii katika Agano la Kale ([yaani, kutokewa, mjadala, mwitikio, ufunuo, agizo], rej. Mwa. 22:1-2, 11-12; 31:11-13; 46:2- 3; Kut 3:2-10; Gerhard Lohfink, The Conversion of St. Paul: Narrative and History in Acts . Chicago: Fransciscan Herald, 1976, uk. 61-69).

Kipinidi cha 1 : Utangulizi

13

B. Tangu tamko la kwanza la Injili (proto-evangelium) hadi Yerusalemu Mpya: ulimwengu uko vitani, Mwa. 3:15; 1 Yoh. 3:8.

1. Msingi wa kito ni katika nafsi ya Mungu mwenyewe, Dan. 4:34-35 – Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; 35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? a. BWANA kama Mwenye Enzi Kuu, Mungu wa Utatu: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu; Zab. 83:18 (NEN) – Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote. b. BWANA Mungu kama Muumba na Aliyefanya vitu vyote; Zab. 24:1-2 – Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. 2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.

2. Ibilisi na wanadamu katika uasi wa hiari dhidi ya utawala na mapenzi yake, walikaidi mapenzi makamilifu ya Mungu na meama yake (Mwa. 3:15).

3. Matokeo: machafuko ya laana, kuingia kwa uovu, kutengwa, na kifo (Rum. 3:23; 6:23).

4. Mapenzi ya Mungu ya ukombozi: kusimamisha tena utawala wa Ufalme wake katika ulimwengu wote.

14

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

a. Kushinda nguvu za uasi na machafuko (Kol. 2:15)

b. Kuurejesha upya uumbaji wake kwa utukufu wake (Isa. 43:7; Ufu. 4:11)

c. Kuwakomboa watu kwa ajili yake mwenyewe (Tit. 2:11-15)

d. Kufunua utukufu wake kupitia kwa Mwanawe na Kanisa (Efe. 1:13–14)

C. Umuhimu wa hadithi ya Kutoka kama kielelezo cha wito mmoja wa Mungu

1. Kama kielelezo cha kibiblia cha kuelewa vipengele vya wito wa Mungu

2. Kama taswira ya simulizi inayosaidia “kuhisi” nguvu ya wito

3. Kama mfano hai unaosaidia kuchambua na kuthamini wito wetu leo

4. Kama sehemu kiungo katika kazi endelevu ya Mungu kwa watu wake.

Maana yake “kuita, kutaja.” Mzizi huu unatokea katika Kiaramu cha Kale, Kikanaani, na Kiugariti, na lugha nyingine za Kisemiti (isipokuwa Kiethiopia). Neno hilo linaonekana katika vipindi vyote vya Kiebrania cha Biblia. Qara’ inaweza kumaanisha “utambulisho wa jina.” Kukipa kitu jina mara nyingi ni ishara ya mamlaka ya mtoa jina kwa kitu hicho, ambalo ndilo jambo la msingi katika matumizi ya kwanza ya qara’ : “Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku” (Mwa. 1:5). Tendo la Mungu la kuumba, “kutoa majina,” na kuhesabu hujumuisha nyota (Zab. 147:4) na vitu vingine

Kipinidi cha 1 : Utangulizi

15

vyote (Isa. 40:26). Alimruhusu Adamu “kuwapa majina” wanyama kama udhihirisho thabiti wa mamlaka na ukuu wa mwanadamu juu ya wanyama (Mwa. 2:19). Ukuu na uteuzi wa kiungu umeenea kwa vizazi vyote, kwani Mungu “aliwaita” wote tangu mwanzo (Isa. 41:4; taz. Amo. 5:8). “Kumwita” au “kumtaja” mtu binafsi kunaweza kubainisha sifa kuu za mtu binafsi (Mwa. 27:36); kunaweza kuhusisha ungamo au tathmini (Isa. 58:13; Isa. 60:14); na kunaweza kuwa namna ya kutambua na kuutambulisha ukweli wa milele (Isa. 7:14). Kitenzi hiki pia kinatumika kuashiria “wito kwa kazi maalum.” Katika Kut. 2:7, Miriamu dadake Musa alimuuliza binti Farao kama aende “kumwita” (kumwagiza kutekeleza kazi) mlezi. Israeli “iliitwa” (kuchaguliwa) na Mungu kuwa watu wake (Isa. 65:12), kama ilivyokuwa kwa watu wa mataifa katika enzi ya Masihi (Isa. 55:5).

~ Vine’s Complete Expository Dictionary, Old Testament utafutaji-neno, toleo tepe katika programu ya kompyuta

D. Hadithi ya Kutoka kama hadithi ya vita: Yehova ni shujaa.

1. Yesu Kristo kama ashindaye ( Christus Victor) : Mwanakondoo ashindaye.

a. Ebr. 2:14 – Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi.

b. 1 Yoh. 3:5 – Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.

c. 1 Yoh. 3:8 – atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

2. Watu wa agano la Mungu walihusika katika vita vya kiroho dhidi ya adui za Mungu.

16

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

a. Ulimwengu: adui wa nje wa mtu wa Mungu (1 Yoh. 2:15-17)

b. Mwili: adui wa ndani wa mtu wa Mungu (Gal. 5:16-23)

c. Ibilisi: adui wa kuzimu wa mtu wa Mungu (Efe. 6:10-18)

3. Silaha za vita vyetu (2 Kor. 10:3-5)

4. Kushindana na wakuu wa giza (Warumi 13)

5. Wawakilishi na mabalozi wa Ufalme (2 Kor. 5:18-21)

E. Wito na Agano: Hadithi ya Kutoka inaeleza mpango wa Mungu kwa kundi hili la watu.

1. Anaita, anawezesha, na kutuma mwakilishi maalum ili kupambana na adui yake.

2. Anaonyesha uwezo na maajabu yake katika hukumu juu ya adui zake.

3. Anawaita, anawaokoa, na kuwafanya upya watu wa agano – anawawezesha ili kwamba waweze kumtukuza na kumwabudu.

Kipinidi cha 1 : Utangulizi

17

 , kaleo¯ Limetokana na mzizi kal -, ambapo kwenye King. ni “ita” na “kelele” (ona B na C, hapa chini), linatumika (a) kwa mtu binafsi, “kumwita mtu yeyote, kualika, kumwagiza kazi,” k.m., Mt. 20:8; Mt. 25:14; linatumika hasa kwa wito wa Kimungu wa kushiriki baraka za ukombozi, k.m., Rum. 8:30; 1 Kor. 1:9; 1 Thes. 2:12; Ebr. 9:15; rej. B na C, hapa chini; (b) linatumika katika utaratibu wa kutoa majina au wito, kazi au nafasi, «kuita kwa jina, kukipa kitu jina»; katika Kauli ya Kutendwa, «kuitwa kwa jina, kuchukua jina.» Kwa hivyo linatoa maana ya ama wito au hatima; muktadha huamua ni kipi, k.m., Rum. 9:25-26; “jina la ukoo,” katika Matendo 15:37, AV, si sahihi (RV, “iliitwa”).

~ Vine’s Complete Expository Dictionary, New Testament utafutaji-neno, toleo tepe katika programu ya kompyuta

F. Kanuni ya Utoshelevu ya wito wa Mungu

1. Kanuni hii inasema: Mungu kamwe haiti mtu au kikundi cha watu kuwa au kufanya chochote bila

kuwapa vipawa, nyenzo, mahitaji, na fursa ya kutimiza wito huo. Flp. 2:12-13 – Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

2. Kanuni hii ilitumika kwa viongozi wa watu wa Mungu: Musa na Yoshua na viongozi wa Agano Jipya.

3. Kanuni hii ilitumika kwa watu wa Mungu: taifa la Israeli na Kanisa.

4. Kila mtu katika Kanisa la Mungu (washirika na viongozi) ameitwa pamoja na wengine ili kuwakilisha sifa, maslahi, na kusudi la Mungu katika maisha yake.

18

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

a. Wito huo unajumuisha watu kutoka mataifa na rangi zote, 1 Kor. 1:24 – bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.

b. Inahitaji mwangaza wa kiroho ili kuuelewa kikamilifu, Efe. 1:18 – macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.

c. Ni lazima tujitahidi kuujua wito wetu ili tuweze kuenenda kama inavyoustahili , Efe. 4:1 – Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa.

d. Hatimaye, wito wetu utahusisha utukufu halisi wa Yesu Kristo , 2 The. 2:14 – aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

G. Asili isiyobadilika ya wito wa Mungu, Rum. 11:29 – Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.

1. Wito na karama za Mungu haziwezi kubatilishwa ( Mungu hatamwondolea mtu wake aliyemwita kazi ile aliyomwitia kufanya ).

2. Wito wa Mungu ndio suala la muhimu zaidi linaloamua mengine yote katika hali zote za kiroho na huduma (Isaya 11).

3. “Wito wa Mungu hauwezi kubatilishwa, si kwamba hauwezi kupingwa.”

Kipinidi cha 1 : Utangulizi

19

II. Wito Mmoja, Madhihirisho Mengi : Njia yenye Mitazamo Mingi katika Kujifunza Wito Halisi

Kwa hiyo twawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu. ~ 2 Wathesalonike 1:11

Je, tunagunduaje wito wetu mahususi katika mwili wa Kristo?

A. Tambua na uelewe vipengele vya wito halisi wa Mungu

1. Wito wa Mungu kwa wokovu : wito halisi unaonyeshwa katika toba na imani kwa Bwana Yesu Kristo.

2. Wito wa Mungu kwa utakatifu : wito halisi unaoonyeshwa kwa kutengwa na Bwana kwa ajili ya kuwa milki yake, kwa kusudi, na furaha yake.

3. Wito wa Mungu kwa uhuru : wito halisi unaoonyeshwa katika ukombozi kutoka katika utumwa wa dhambi na dini ili kuingia katika maisha ya upendo thabiti kwa Mungu na kwa wengine.

4. Wito wa Mungu kwa jumuiya : wito halisi unaonyeshwa katika kufanyika sehemu ya jumuiya ya kiagano ya Mungu na kuiwakilisha jumuiya hiyo.

B. Tambua na uelewe majukumu ya wito wa Mungu

1. Wito wa Mungu kwa ajili ya kutumika : wito halisi unaonyeshwa katika kutumia karama, rasilimali, na fursa za mtu kulijenga Kanisa na kuvuna ulimwengu.

2. Wito wa Mungu wa kuteseka : wito halisi unaonyeshwa kwa utayari wa kujitolea, kupambana, na kuvumilia kwa gharama yoyote ili kutimiza mapenzi ya Mungu.

20

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

C. Tambua na uelewe wito wa Mungu kwa maisha yetu yote , pamoja na wito wake maalum kwa wale walioitwa kuandaa na kuwajenga watu wake.

1. Wito maalum wa Mungu na huduma tano za uwezeshaji katika Waefeso 4 : mitume, nabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu.

2. Wanaume na wanawake wa uchaguzi na ufunuo wa Mungu mwenyewe.

3. Karama za vipawa vitokanavyo na upaji na uwepo wa Mungu mwenyewe.

D. Bwana Mwenye Enzi Kuu juu ya ulimwengu wote anawaita watu kwake, na anawaita ili wawe wawakilishi wake.

1. Alikusudia wito huu kabla ulimwengu haujaanza, 2 Tim.1:9 (SRUV) – ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu kabla ya wakati kuanza.

2. Ni wito shirikishi wa kimbingu, Ebr. 3:1 – Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu.

3. Kwa hiyo, wajibu wetu ni kuishi katika namna itakayofanya wito na uteule wetu kuwa thabiti katika mioyo yetu wenyewe , 2 Pet: 1:10 – Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.

Kipinidi cha 1 : Utangulizi

21

Sala na Ukiri kwa Mungu

Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema. 19 Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari. 20 Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Ibrahimu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale. ~ Mika 7:18-20

Kipindi cha 2 Wito wa Wokovu Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Wokovu

Rum. 8:28-30 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye kwa kusudi lake. 29 Maana wale awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza. 2 The. 2:14 Aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo 1 Kor. 1:2 Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu. Flp. 3:14 Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu

Je, tunaweza kujifunza nini katika kutazama vipengele hivi vya wito wa Mungu?

• Ni vipengele jumuishi kwa maana kwamba vinamgusa kila mtu ndani ya jumuiya ya kiagano (yaani, watu binafsi, familia, na watu wote) kwa ukamilifu, katika nyanja zote za maisha. • Vimeungamanishwa kwa maana ya kwamba vinaamua na kufafanua kila kitu kingine kinachohusishwa na utekelezaji wa wito wa Mungu. • Ni vya jumla kwa maana kwamba vinatumika kwa watu binafsi na familia zote kwa usawa, bila kujali wito fulani ambao Mungu anao kwa maisha yao binafsi.

I. Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Wokovu

Yesu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Na Bwana wa ulimwengu wote anaamrisha kila mtu kumfuata. Wito wake kwa Petro na Andrea (Mt. 4:18-19) na kwa Yakobo na Yohana (Mt. 4:21) ulikuwa ni amri. “Nifuate” daima imekuwa amri, kamwe si mwaliko (Yohana 1:43). Yesu hakuwahi kumsihi mtu amfuate. Alikuwa wazi sana. Alimkabili mwanamke kisimani na uzinzi wake, Nikodemo na kiburi chake cha kiakili na Mafarisayo kwa kujiona kwao kuwa wenye haki. Hakuna anayeweza kutafsiri “. . . Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” kama ombi (Mt. 4:17). Yesu aliamuru kila mtu aachane na mambo ya ubinafsi, aache dhambi yake na kumtii kabisa. Yule mtawala kijana tajiri alipokataa kuuza vitu vyote na kumfuata (Mt. 19:21) Yesu hakumkimbilia akijaribu kufanya mapatano ya kupata muafaka naye. Hakuwahi kushusha kiwango chake. Yesu alisema tu, “Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate . . .” (Yohana 12:26, NEN). . . . Basi ni lini unakuwa Mkristo, mwanafunzi wa Kristo? Unapopita mbele kuitikia wito wa muhubiri? Unapopiga magoti mbele ya madhabahu? Unapolia kwa dhati? Si lazima. Wafuasi wa awali wa Kristo walikuwa wafuasi walipomtii, wakati “walipoiacha mara moja mashua yao na baba yao, wakamfuata” (Mt. 4:22). Kutii amri ya Kristo, “Nifuate,” husababisha kujikana. Ukristo bila kujikana ni falsafa ya kufikirika tu. Ni Ukristo bila Kristo. ~ Keith Phillips. The Making of a Disciple . Old Tappan, NJ: Fleming H. Revell Company, 1981. uk. 16-17.

23

24

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

A. Ufafanuzi wa wito wa wokovu katika hadithi ya Kutoka

1. Wito maalum wa Musa, Kut. 3:10-12 – Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri. 11 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri? 12 Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa

umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.

2. Mapambano ya Mungu na Farao kupitia Musa , Kut. 7:15-18 – Mwendee Farao asubuhi; tazama, atoka kwenda majini; nawe simama karibu na ufuo wa mto ili upate kuonana naye; na ile fimbo iliyogeuzwa kuwa nyoka utaichukua mkononi mwako. 16 Nawe umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, amenituma nije kwako, kusema, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia jangwani; nawe, tazama! Hujasikia hata sasa. 17 Bwana asema, Katika jambo hili utanijua ya kuwa mimi ndimi Bwana; tazama, nitayapiga haya maji yaliyo mtoni kwa fimbo hii niliyo nayo mkononi mwangu, nayo yatageuzwa kuwa damu. 18 Na hao samaki walio mtoni watakufa, na huo mto utatoa uvundo; nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni. 3. Ugumu wa moyo wa Farao unapelekea kwenye hukumu ya Mungu juu ya Misri kupitia miujiza ya kimungu, ishara na maajabu, Kut. 5:1-2 – Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani. 2 Farao akasema, Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui Bwana, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.

4. Mungu kujikombolea watu wake kwa kusudi la ibada na utumishi, Kut. 3:19 – Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu.

Kipindi cha 2 : Wito wa Wokovu

25

B. Kanuni kwa watu wa Mungu leo

1. Muhtasari wa kusudi la Mungu la ukombozi

a. Mungu pekee ndiye Muumba na Mwenye Enzi Kuu juu ya ulimwengu wote mzima.

(1) Zab. 92:8 – Bali Wewe, Bwana, U Mtukufu hata milele.

(2) Isa. 54:5 – Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.

b. Mungu amedhamiria kuushinda uasi wa shetani (1 Yoh. 4:4).

c. Mungu amekusudia kurejesha na kukomboa uumbaji wake, Rum. 8:19-21 – Kwa maana

viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; 21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu

d. Mungu atauthibitisha upya utawala wake kwa kuwaokoa watu kwa ajili yake mwenyewe, Tit. 2:11-15.

e. Mungu atajumlisha vitu vyote katika Mwanawe, Masihi na Bwana, Efe. 1:9-10 – akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. 10 Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;

26

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

2. Ahadi ya wazi ya wokovu

a. Hadithi ya Utukufu wa Mungu na nafsi ya Yesu wa Nazareti (Lk 4:16-18 rej. Isa. 61:1-4).

b. Injili ya Ufalme, Mk. 1:14-15 – Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, 15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.

c. Tubuni dhambi zenu na kuamini Habari Njema.

(1) Mdo 2:38 – Petro akawaambia, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” (2) Mdo. 20:21 – nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.

3. Mwitikio thabiti wa ufuasi (Lk 14:26-33)

a. Wa haraka, Mt. 4:19-22 – Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. 20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 21 Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. 22 Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata. b. Wa bila masharti, Lk. 9:23-26 – Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi

Kipindi cha 2 : Wito wa Wokovu

27

yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha . 25 Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe? 26 Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu

Wito wa wokovu pia, wakati huo huo, ni wito wa kupokea msamaha wa Mungu kwa njia ya neema ya Yesu Kristo, na kuitikia neema hiyo kama mfuasi, kumkiri Yesu kuwa Bwana. Rum. 10:8-13 Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. 9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. 11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. 12 Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; 13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka

c. Wenye kubadilisha, Yn. 8:36 – Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.

C. Mifano halisi kuelezea wito wa wokovu

1. Mitume Yohana na Yakobo: hadithi za wito wa Injili (Mt. 4:18-22).

2. Zakayo, mtoza ushuru (Lk. 19:1-10).

3. Sauli wa Tarso, Mdo. 9:15-16 – Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. 16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.”

D. Ufahamu wa kipekee kwa viongozi wa kiroho: Ni nani anayetoa wito?

1. Mungu ndiye hutoa wito, wa wokovu na wa utumishi pia. Chanzo cha wito wa Mung si mtu binafsi wala Kanisa, 1 Kor. 1:24-28.

2. Ingawa wito unaweza kuja kwa njia nyingi kama ambavyo pia kuna wahudumu wengi wa kuupokea, wito halisi wa huduma daima utajumuisha uwepo, nguvu, na karama za Roho.

28

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

a. Uwepo endelevu wa Mungu, Roho Mtakatifu (Mdo 13:2).

b. Karama na nguvu za Roho (Mdo 1:8; 6.3).

3. Mungu ndiye mwanzilishi wa wito kwa kila mtu ambaye anamwita katika huduma.

a. Ezekieli, Eze. 2:1-8

b. Mitume, Mt. 4:18-22

c. Kuhani mkuu, Ebr. 5:4

d. Paulo

(1) Mdo. 13:2

(2) Rum. 1:1

(3) Gal. 1:1-.

4. Kama Bwana wa mavuno na kichwa cha Kanisa, Yesu Kristo peke yake ndiye anayegawa na kuwateua viongozi kwa kazi yao miongoni mwa watu wa Mungu (Efe. 4:7-11).

5. Ingawa Mungu peke yake ndiye anayetoa wito wa huduma, wito halisi wa uongozi utaonyeshwa kwa uzoefu na kuthibitishwa na mamlaka halali ya kiroho .

a. Paulo, Gal. 2:6-10

b. Timotheo, 2 Tim. 1:14

Kipindi cha 2 : Wito wa Wokovu

29

Injili ya Tano

Hii naiita injili ya tano. Tuna Injili za Mt. Mathayo, Mt. Marko, Mt. Luka, na Mt. Yohana, na sasa ya tano, Injili ya Watakatifu Waumini wa Kiinjili. Injili hii ya Waumini wa makanisa ya Kiinjili imechukuliwa kutoka katika aya za hapa na pale katika Injili nyingine nne. Mara nyingi huwa tunachukua mstari mmoja hapa, mstari mmoja pale, aya zote zinazotoa jambo fulani tunalolitamani, mistari yote yenye ahadi kama Yohana 3:16 na Yohana 5:24, tukiweka mistari hii yote pamoja ili kuunda theolojia ya utaratibu juu ya wokovu. Halafu tunasahau mistari mingine, matakwa na maagizo ya Yesu Kristo. Hii ni injili ya tano, injili ya ahadi, injili inayomtambulisha Yesu kama Mwokozi binafsi – pekee. Ni nani aliyeturuhusu kumwasilisha Yesu kama hivi au vile na si kama alivyo kiuhalisia? Hebu tufikiri, wanandoa wachanga wanafunga ndoa. Na mchungaji anapomuuliza bwana arusi, “utamchukua mwanamke huyu kuwa mke wako?” kijana huyo anasema, “Mchungaji, ninamkubali msichana huyu kama mpishi wangu binafsi, msafisha vyombo, na kijakazi.” Hivi msichana huyo angesemaje? Angesema, “Subiri kidogo. Nitaenda kupika, ndio. Na nitaenda kuosha vyombo. Nitaenda kusafisha nyumba. Lakini mimi si mjakazi. Nitakuwa mke wako, na lazima pia unipe upendo wako, moyo wako, nyumba yako – kila kitu.» Hiyo ndio ndoa! Ndivyo ilivyo pia kwa Yesu. Ni kweli yeye ni Mwokozi. Kisha tunakuwa wa kiroho na kumkubali kama mponyaji pia. Subiri kidogo. Yeye yuko kama alivyo. Hatuwezi kumkata Yesu vipande vipande na kuchukua kipande tunachokipenda zaidi. Sisi ni kama watoto wanaopewa mkate na jemu. Wanakula jemu na kukurudishia mkate. Kisha unaweka jemu zaidi juu yake na wanalamba jemu tena na kukupa mkate. Hivyo ndivyo tunavyotaka kufanya na Yesu. Tunataka kuchukua jemu na kurudisha mkate. Tunapaswa kula mkate na jemu. Mbingu zinaweza kuwa jemu, lakini Bwana Yesu ndiye Mkate wa Uzima.

~ Juan Carlos Ortiz. Call to Discipleship . Plainfield, NJ: Logos International Press, 1975. uk. 55-56.

II. Kuitikia Wito

A. Matokeo yake kwa huduma ya mjini

1. Mungu ndiye anayetawala, na anafanya kila kitu kwa kusudi lake kuu. Hakuna eneo, mtaa, jamii, jiji, au mkoa unaomtisha , Isa. 44:6-7 – Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; “Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. 7 Naye ni nani kama mimi atakayeita,

30

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze.”

2. Watu wamepotea na pasipo ukombozi ambao Mungu pekee hutoa kupitia Yesu Kristo, wataangamia, Yn. 3:16, 36.

3. Mungu anawaita watu wote kila mahali watubu na kumwamini Yesu Kristo, Mdo. 17:30-31 – Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. 31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu. 4. Wahudumu wa kweli wa mijini, kama Musa, wamekutana na “kijiti kinachowaka moto”; hivyo ni lazima watakuwa wameitikia wito wa Mungu katika toba ya kibinafsi na imani ( huwezi kutoa usichokuwa nacho; huwezi kupoteza kile ambacho hujawahi kuwa nacho ).

5. Wito wa kuokolewa pia ni wito wa ufuasi: mwitikio wa haraka kwa Yesu, usio na masharti, na ubadilishao.

B. Kuhusianisha somo na maisha yako leo

1. Je, ninamtambua BWANA kuwa Muumba wangu na Muumba wa vitu vyote?

2. Je, ninaelewa na kuamini muhtasari wa Biblia wa Hadithi ya utukufu wa Mungu?

3. Je, nimetubu na kumwamini Yesu Kristo kama Masihi na Bwana wa wote?

Kipindi cha 2 : Wito wa Wokovu

31

4. Je, niko tayari sasa, papa hapa na sasa hivi, kuachilia vyote nilivyo na nitakavyokuwa kumtii Yesu Kristo kama Bwana wa maisha yangu?

Sala na Ukiri kwa Mungu

Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani. 2 Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono. 3 Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara. 6 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; 7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. ~ Isaya 55:1-3, 6-7

Kipindi cha 3 Wito wa Utakatifu Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Utakatifu

Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.

~ 1 Wathesalonike 4:7

Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;

~ Waefeso 4:1

Ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.

~ 1 Wathesalonike 2:12

Uongozi wa kiroho unahitaji watu waliojazwa na Roho. Sifa nyingine ni muhimu; lakini kujazwa na Roho ni jambo la lazima. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni hadithi ya watu walioanzisha Kanisa na kuongoza shughuli ya kimishenari. Ni jambo la muhimu kiasi kikubwa mno kwamba sifa kuu ya wale ambao walitakiwa kuchukua hata nyadhifa za chini za madaraka katika Kanisa la kwanza ilikuwa kwamba wawe watu “waliojaa Roho Mtakatifu.” Maafisa hawa walipaswa kujulikana kwa uadilifu na uwezo wa kufanya maamuzi, lakini hasa kwa hali yao ya kiroho. Mtu anaweza kuwa na akili nzuri na kuwa na ustadi wa kiutawala. Lakini bila kuwa mtu wa rohoni ( sic ) hana uwezo wa kutekeleza uongozi halisi wa kiroho. Nyuma ya shughuli zote za mitume kulikuwa na utendaji mkuu wa Roho. Kama msimamizi mkuu wa Kanisa na mwanamkakati mkuu wa shughuli za kimishenari anajulikana kila mahali. . . . Uteuzi wa viongozi wa Ufalme haupaswi kuongozwa na hekima ya ulimwengu, mali, au hadhi. Jambo kuu la kuzingatia ni hali ya kiroho. Kanisa au shirika la kimisheni linapofuata seti tofauti ya vigezo, kimsingi huko ni kumwondoa Roho kutoka kwenye uongozi.

~ J. Oswald Sanders. Spiritual Leadership . 2nd Edition. Chicago: Moody Press, 1994. uk. 79-80.

33

34

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

I. Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Utakatifu

A. Ufafanuzi wa wito wa utakatifu katika hadithi ya Kutoka

1. Kuwekwa wakfu kwa watu kwa ajili ya Mungu mwenyewe

a. Law. 11:44 – Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.

b. Law. 19:2 – Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu.

c. Law. 20:7 – Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

2. Kuwekwa wakfu kwa mzaliwa wa kwanza (pamoja na kuadhimisha Pasaka), Kut. 13:11-16 – Itakuwa hapo Bwana atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, na kukupa, 12 ndipo utamwekea Bwana kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao waume watakuwa ni wa Bwana. 13 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana kondoo; na kwamba hutaki kumkomboa, utamvunja shingo; na kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa. 14 Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, Bwana alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake; 15 basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea Bwana wote wafunguao tumbo, wakiwa waume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa. 16 Jambo

Kipindi cha 3 : Wito wa Utakatifu

35

hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa Bwana alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.

3. Kutolewa kwa Torati Sinai: Agano la Mungu na watu wake , Kut. 19:3-6 – Musa akapanda kwa Mungu, na Bwana akamwita toka mlima ule, akisema, “Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno haya; 4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.”

a. Utambulisho wao na jumuiya yao wenyewe

b. Nidhamu, utaratibu, na utawala wao wenyewe

c. Hatima mpya: watu wa Masihi wakitoa ushahidi kwa mataifa yanayowazunguka kuhusu uaminifu wa agano la Mungu.

 , hagios Neno linalotokana na mzizi mmoja na hagnos (hupatikana katika hazo , “kutoa heshima ya hali ya juu”), kimsingi humaanisha “kutengwa” (miongoni mwa Wayunani, kuwekwa wakfu kwa miungu), na kwa hiyo, katika Maandiko katika maana yake ya kiadili na kiroho, kutengwa na dhambi na hivyo kuwekwa wakfu kwa Mungu, takatifu. (a) Linamwelezea Mungu (kama “Mtakatifu” kabisa, katika usafi wake, ukuu na utukufu wake): Baba k.m., Lk. 1:49; Yn. 17:11; 1 Pet. 1:15, 16; Ufu. 4:8; Ufu. 6:10; Mwana, k.m., Lk. 1:35; Mdo. 3:14; Mdo 4:27, 30; 1 Yoh. 2:20; Roho , k.m., Mt. 1:18 na mara nyingi katika Injili zote, Matendo, Warumi, 1 na 2 Wakorintho, Waefeso, 1 Wathesalonike; pia katika 2 Tim. 1:14; Tit. 3:5; 1 Pet. 1:12; 2 Pet. 1:21; Yud. 1:20. (b) Linatumika kwa watu na vitu (tazama hapa chini) kwa kadiri wanavyojitoa kwa Mungu. Kwa hakika sifa yoyote inayohusishwa na Mungu, mara nyingi

36

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

huwasilishwa kwa njia ambayo inahusisha matakwa ya Kiungu juu ya mwenendo wa waumini. Hawa wanaitwa hagioi, “watakatifu,” yaani, “waliotakaswa”. Utakatifu huu si ambao mtu anaweza kuufikia kwa kutimiza vigezo fulani vya kidini, ni hali ambamo Mungu katika neema huwaita wanadamu; hata hivyo waamini bado wanaitwa kuendelea kujitakasa (kulingana na wito wao, 2 Tim. 1:9), wakijitakasa wenyewe kutoka kwenye unajisi wote, wakiacha dhambi, wakiishi maisha “matakatifu,” 1 Pet. 1:15; 2 Pet. 3:11, na kuwa na ushirika na Mungu katika utakatifu wake. Kwa hiyo, katika lugha ya picha watakatifu wanatajwa kuwa “hekalu takatifu,” 1 Kor. 3:17 (kanisa la mahali); Efe. 2:21 (Kanisa zima), rej. Efe. 5:27; “ukuhani mtakatifu,” 1 Pet. 2:5; “taifa takatifu,” 1 Pet.2:9. “Ni wazi kwamba hagios na maneno ya jamii yake . . . yanaeleza jambo fulani la zaidi na la juu zaidi kuliko hieros , takatifu, inayohusianishwa na Mungu kwa nje; . . . jambo zaidi ya semnos , inayostahili, yenye heshima; jambo zaidi ya hagnos , safi, isiyo na unajisi. Hagiosis . . . katika namna pana zaidi. . . . Ni tabia ya kumfanania Mungu.”

~ G.B. Stevens, in Hastings’ Bible Dictionary Vine’s Complete Expository Dictionary, Old Testament utafutaji-neno, toleo tepe katika programu ya kompyuta

B. Kanuni kwa watu wa Mungu leo

1. Mungu ameifunua nafsi yake kama mtakatifu na aliyetengwa, 1 Pet. 1:14-19 – Kama watoto wa kutii

msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. 18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.

a. Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ni Mungu mtakatifu.

Kipindi cha 3 : Wito wa Utakatifu

37

b. Kusudi la Mungu ni kuusimamisha upya utakatifu wake katika ulimwengu wake wote.

c. Utawala wa ufalme wa Mungu umetofautishwa na kutengwa na mfumo wa ulimwengu wenye choyo, tamaa, na kiburi.

2. Mungu amejikombolea watu wake watakatifu; tumeitwa kuwa watakatifu, 1 Kor. 1:2 – Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.

a. Limenunuliwa kama mali maalum ya Mungu mwenyewe (Tit. 2:14).

b. Limetengwa na ulimwengu liwe la Mungu mwenyewe kwa ajili ya mapenzi yake na kusudi lake (Ufu. 4:11; 2 Tim. 1:9).

c. Linakusudiwa kuakisi utakatifu wa utukufu wa Mungu kupitia maisha yake na uwepo wake wa kinabii na kuhubiri kwake, 1 Pet. 2:9-10 – Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

3. Watu wa Mungu wanapaswa kukumbatia na kuyathamini mapokeo ya kinabii na kitume ambayo juu yake imani na utendaji wetu umejengwa.

a. 2 The. 2:15 – Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.

38

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

b. Efe. 2:19-21 – Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.

C. Mifano halisi kuelezea wito wa utakatifu

Wito wa utakatifu ni wito kwa watu wa Mungu kuwa mali yake yenye thamani ili kuakisi ukuu na utukufu wake katikati ya mataifa. 1 Pet. 2:9-10 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

1. Yoshua na majeshi ya Mungu huko Yeriko, Yos. 3:5 – Yoshua akawaambia watu, “Jitakaseni; maana kesho Bwana atatenda mambo ya ajabu kati yenu.”

2. Waongofu wa Efeso, Mdo. 19:17-20 – Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa. 18 Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. 19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu. 20 Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu. 3. Waamini wa Thesalonike, 1 The. 1:6-8 – Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu. 7 Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya. 8 Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software