Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 7 Wito wa Mateso Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Mateso
Na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;
~ Waebrania 5:8
Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; 30 mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.
~ Wafilipi 1:29-30
Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, 22 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi..
~ Matendo 14:21-22
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
~ 1 Petro 5:10
Mwanzoni kabisa mwa somo lolote la uongozi wa kiroho, kanuni hii kuu lazima izingatiwe kikamilifu: Ukuu halisi, uongozi wa kweli, unapatikana katika kujitoa katika huduma kwa wengine, na si katika kubembeleza au kuwashawishi wengine wakutumikie. Huduma ya kweli haikosi gharama. Mara nyingi huja na ubatizo wa maumivu ya mateso. Lakini kiongozi wa kweli wa kiroho anazingatia huduma ambayo anaweza kumtolea Mungu na watu wengine, si kwa habari ya manufaa ya cheo cha juu au cheo kitakatifu. Lazima tulenge katika kuwekeza zaidi maishani kuliko tunavyochukua.
~ J. Oswald Sanders. Spiritual Leadership . Toleo la 2. Chicago: Moody Press, 1994. uk. 15.
81
Made with FlippingBook Digital Publishing Software