Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 7 : Wito wa Mateso
83
3. Kustahimili kunidhamishwa na Mungu nyikani kwa sababu ya kutoamini na kurudi nyuma (Hes. 14:26-35)
4. Kupigana katika vita vitakatifu dhidi ya maadui wa Mungu kulingana na njia ya Mungu ya kuweka wakfu na baraka (Yos. 1:1-9).
5. Kudumu katika uaminifu kwa agano usoni pa ibada ya sanamu, uonevu, kurudi nyuma, na makosa (Yos. 24:14-24).
1 Pet. 4:12-16 Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa Mungu anawakalia. 15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. 16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.. kuwa Roho wa utukufu na wa
B. Kanuni kwa ajili ya watu wa Mungu leo
1. Mahali pa unyenyekevu: kushiriki nia ya Yesu , Flp. 2:5-8 – Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
2. Mapambano dhihi ya uovu: kushiriki mapambano ya Yesu
a. Mt. 10:24-25 – Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. 25 Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
b. Mt. 12:30 – Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software