https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 1 1

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

kwa imani katika Yesu Kristo, wanafanyika washiriki wa jamii ya ufalme wake ambao wataishi pamoja naye milele. ³ Taswira ya Utume kama Vita vya Milki pengine ndiyo taswira yenye nguvu zaidi ya utume katika Maandiko, na inahusika moja kwa moja na kuanzishwa na kutangazwa kwa utawala wa ufalme wa Mungu katika Yesu wa Nazareti. ³ Muhtasari mfupi wa taswira ya vita katika Maandiko unaanza na Yahweh kama muumbaji na mtegemezaji wa yote. Wakati fulani katika nyakati za kale na za mbali, siri ya kuasi ilitokea (yaani, uasi wa kishetani huko mbinguni), ambao ulisababisha majaribu na anguko la wanadamu, na laana. Hata hivyo, Mungu aliweka uadui kati ya Uzao wa mwanamke na nyoka, na kwa ukuu na fadhili akaahidi kuponda kichwa cha nyoka kupitia Uzao wa mwanamke. Kama matokeo ya Anguko, ulimwengu uko vitani na Mungu amejitangaza kuwa anapigana na nyoka na wale walio upande wake. ³ Baadhi ya mambo makuu ya Mungu kama shujaa wa kiungu ni pamoja na picha ya Mungu akishinda uovu iliyofananishwa na mto na bahari, na vilevile Mungu akiwa mtu wa vita akimshinda Farao na majeshi yake, na kuwaongoza watu wake katika ushindi juu ya mataifa ya nchi ya ahadi kama Bwana mkuu wa majeshi. Kwa bahati mbaya, Bwana pia alilazimika kupigana na watu wake mwenyewe kwa sababu ya kutotii na uasi wao. Pia, manabii wa Israeli walimzungunzia Mungu kama Shujaa wa kiungu ambaye hatimaye kupitia Masihi wake angeharibu uovu wote mara moja, milele. ³ Mungu, kupitia ahadi yake ya Masihi ambaye ni mwana wa Daudi, alifunua kusudi lake la kuandaa mfalme ambaye angerudisha utawala kwa watu wake, kutawala mataifa kwa haki na uadilifu, na kuleta ujuzi wa Mungu duniani kote akiwa Bwana na Mfalme. Utawala huu wa Kimasihi umezinduliwa katika nafsi ya Yesu, mrithi kutoka katika ukoo wa Daudi ambaye anarudisha utawala wa Mungu. ³ Kupitia vipengele mbalimbali vya kuzaliwa kwa Yesu, mafundisho yake, miujiza yake, kutoa pepo, matendo yake, kifo na ufufuo wake, ni dhahiri kwamba Ufalme wa Mungu sasa uko hapa, tayari upo katika maisha ya Kanisa. Ufalme umekwisha kuja, na bado haujakamilika; ijapokuwa Ufalme umekuja katika utimilifu wa ahadi ya Kimasihi katika nafsi ya Yesu, utakamilika tu wakati wa Kuja kwake Mara ya Pili, pale udhihirisho kamili na wa mwisho utakapotokea.

2

Made with FlippingBook Annual report maker