https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 1 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
sanamu, na ukosefu wa haki, hadi hukumu ya Mungu na uhamisho na utumwa wa Israeli (Ufalme wa Kaskazini), na Yuda (Ufalme wa Kusini). ³ Kurudi kwa watu wa Mungu katika nchi kulianza kwa amri na ruhusa ya Mfalme Koreshi ya kuingia tena katika nchi, ambayo ilitekelezwa kupitia Ezra, Zerubabeli, na Nehemia. Mungu aliwaahidi watu wake kwamba angefanya nao agano jipya, ambalo halikuwa kwa msingi wa utii na uaminifu wao bali kwa kuandika sheria yake mioyoni mwao na kuwapa roho mpya. Hatimaye, watu wa Mungu wangerudishwa kwake, na siku moja angecheza na kushangilia juu ya watu wake kama bwana-arusi afanyavyo juu ya bibi-arusi wake. ³ Vidokezo vya tumaini na ahadi ya agano jipya vimejumuishwa katika agano la Mungu na Ibrahamu, na matarajio yake ya kujumuishwa kwa mataifa. Katika Yesu Kristo, taswira ya bwana-arusi imepanuliwa na kukamilishwa. Yesu sasa amekuwa chanzo na uzima wa Kanisa, bibi-arusi wake mpya, na Yohana Mbatizaji, mtangulizi wake, amekuwa rafiki wa bwana-arusi. ³ Muundo kamili wa watu wa Mungu ulifunuliwa kupitia kufunuliwa kwa siri kupitia mitume na manabii, kwamba Mataifa ni warithi pamoja na Wayahudi katika ahadi ya agano jipya la Mungu, na kupitia hilo, wanakaribishwa kama washiriki wa jamii mpya ya watu wa Mungu na bibi-arusi wa Kristo. ³ Mataifa wote (kama Wayahudi) wanakaribishwa katika mwili (Kanisa) na bibi-arusi wa Kristo kwa imani, kuoshwa katika damu yake na kujumuishwa katika Kanisa la Mungu. Mataifa hawana haja ya kukana utambulisho wao wa kitamaduni kama ilivyofafanuliwa katika Baraza la Yerusalemu (rej. Mdo. 15), na sasa kiini cha huduma zote za kitume ni kuwatayarisha watu wa Mungu kama bibi-arusi, ambaye Kristo atampokea wakati wa kuja kwake, bila mawaa machoni pake. ³ Mapenzi ya kiungu yatakamilika kwa kushuka kwa Yerusalemu Mpya kutoka mbinguni, makao ya Mungu na watu wake, ambao watajitambulisha kikamilifu na Kristo, bwana-arusi kwa kubadilishwa na kufanana naye, kuwa warithi pamoja naye, wakiwa katika uwepo wake milele kama watawala pamoja naye. ³ Kwa habari ya utume, vipengele vikuu vya mapenzi ya kiungu ni hivi: Mungu anavuta watu kutoka katika mataifa yote kwa ajili yake, ambao ni pamoja na Wayahudi na mataifa. Kwa hiyo, utume ni kazi ya kueneza ujumbe huu wa Mungu kuchagua watu kutoka katika mataifa yote ambao,
2
Made with FlippingBook Annual report maker