https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 0 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
watamtii, “Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.” Anafanya hivi mara nyingi katika historia ya Israeli, akijitokeza kwa namna mbalimbali na kutumia njia tofauti tofauti kushinda vita. Mara nyingi Mungu anatumia nguvu za asili, uumbaji wake mwenyewe, kama silaha zake. Wakati wa kuvuka Bahari ya Shamu wakati Israeli inaokolewa na Misri kuhukumiwa, Mungu anatumia upepo kurudisha nyuma maji ya Bahari ili kuwaruhusu Waisraeli wavuke ng’ambo ya pili na kisha kuyaangusha maji kuwaua Wamisri (Kut. 14 na 15). Baadaye, Yoshua anapopigana na muungano wa wafalme wa kusini mwa Kanaani, Mungu anatumia mvua ya mawe makubwa kuwaua adui na kusababisha jua lisimame angani ili kuwe na mwanga wa mchana zaidi kwa lengo la kumaliza vita (Yos. 10:1-15). Wakati mwingine Mungu anatumia jeshi lake la mbinguni kupigana na adui za Israeli. ~ Leland Ryken. The Dictionary of Biblical Imagery . (toleo la kielektroniki) Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 211. Somo hili linashughulika na taswira mbili muhimu zaidi katika Maandiko yote, na sio tu kuhusiana na suala la utume. Taswira za Utume kama Mapenzi ya Enzi na Utume kama Vita vya Milki zinagusa mada muhimu kweli ambazo zina umuhimu mkubwa kwa ufahamu wetu wa kazi ya Masihi na Kanisa. Tunaweza kusema kwa urahisi kwamba kufahamu mada hizi ndio namna kuu ya kufahamu maana sio tu ya utume, bali pia utambulisho wa Kanisa na kazi ya Kanisa. Kwa sababu hiyo, kagua dhana hizi kwa uangalifu, na uhakikishe kuwa unaweza kuziunga mkono kwa kutumia Maandiko. ³ Mapenzi ya kiungu kati ya Mungu na watu wake ni mojawapo ya sababu kuu za utume katika Maandiko Matakatifu, yaani, azimio la Mungu la kuvuta watu kutoka ulimwenguni ili wawe milki yake mwenyewe, milki iliyotimizwa na kukamilishwa katika upendo wa Yesu kwa Kanisa lake. ³ Dhana ya bwana-arusi na bib-arusi ni maarufu katika Agano la Kale, inahusiana na wazo la muungano wa kijamii, furaha, na shangwe katika Maandiko, pia inatumika kama taswira ya msingi ya uhusiano wa Mungu na watu wake (kama inavyoonekana katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora). ³ Dhana ya Israeli kama bibi-arusi wa Mungu inaanza na uhusiano wa Mungu na Israeli katika asili yake duni na ya kupuuzwa, kwa uteuzi wa neema wa Mungu, uchumba na ndoa, uzinifu wa Israeli, kutoamini na ibada za
2
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook Annual report maker