https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 0 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
6. Taja kwa ufupi njia ambazo katika hizo ahadi ya Masihi imezinduliwa katika nafsi ya Yesu, mrithi kutoka katika ukoo wa Daudi ambaye anarudisha utawala wa Mungu. Namna gani mambo mbalimbali yanayohusu kuzaliwa kwake, mafundisho, miujiza, kutoa pepo, matendo yake, kifo chake, na ufufuo wake yanaonyesha kwamba Ufalme wa Mungu ulioahidiwa sasa uko hapa, tayari uko katika maisha ya Kanisa? 7. Elezea ni kwa namna gani Ufalme wa Mungu unaweza kusemwa kuwa “tayari upo” lakini “haujakamilishwa.” Kwa nini tofauti hii ni muhimu kukumbuka kila wakati tunapojadili kazi ya Yesu Kristo katika enzi hii ya sasa? 8. Ni katika maana gani tunaweza kusema kwamba Kanisa la Yesu Kristo leo katika enzi hii ni ishara na kionjo cha awali cha Ufalme uliopo? Ni katika maana gani Roho Mtakatifu, anayekaa ndani ya Kanisa, anatoa uthibitisho kwamba Ufalme wa Mungu kwa hakika umefika kupitia Yesu Kristo? Je, Kanisa sasa limeidhinishwa kufanya nini kwa niaba ya Kristo kwa ajili ya Ufalme? 9. Ni zipi athari kuu za taswira ya Utume kama Vita vya Milki kwa umisheni? Kwa msingi wa Mungu kuthibitisha tena utawala wake juu ya ulimwengu wote katika Yesu Kristo, wamishenari wanapaswa kufanya nini na wanapaswa kuendeshaje kazi na huduma zao miongoni mwa waliopotea? 10. Soma nukuu ya Ryken hapa chini. Kwa nini ni muhimu kuona taswira hizi mbalimbali za Mungu kuwa zinahusiana na kushikamana, badala ya kutofautiana na kutengana? Je, Ryken anatusaidiaje kuunganisha picha hizi tunapozitumia kuelewa Mungu ni nani na matendo yake ulimwenguni (ambayo, kwa hakika ndiyo misingi ya kazi ya utume leo)?
2
Mungu wa Ahadi pia ni Mungu wa Vita
Mungu anapoonekana kama Shujaa wa kiungu katika Agano la Kale, mara nyingi ni tukio la Yeye kuja kuwaokoa watu wake na mkono wa adui zao. Hili lilitokea tangu wakati wa kuvuka Bahari ya Shamu hadi mwishoni mwa historia ya Israeli. Taswira ya Shujaa wa kiungu imeunganishwa kwa karibu na wazo la ‘agano’ katika Agano la Kale. Mungu anajifunua kama Mfalme kupitia mapatano ya kiagano kisha anaahidi kuwalinda watu wake dhidi ya hatari na vitisho vya adui zao. Tunaweza kuona hili katika ahadi ya baraka ambayo Mungu aliitoa ikiwa watu watatii sheria ya agano. Katika Kumbukumbu la Torati 28:7, Mungu Mfalme anaahidi kwamba ikiwa Israeli
Made with FlippingBook Annual report maker