https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 0 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kufanya marudio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video. Katika sehemu yetu ya mwisho tumepitia kwa ufupi kile ambacho kinaweza kuchukuliwa kuwa mojawapo ya mada na taswira unganishi na zenye nguvu kuhusu utume katika Biblia nzima : Taswira ya Utume kama Vita vya Milki ambayo imejikita katika kuthibitisha tena utawala wa Mungu katika nafsi ya Yesu wa Nazareti. Taswira hii inaangazia wazo la Shujaa wa kiungu katika Biblia, mada ambayo inapata kilele chake katika Yesu, Masihi wa Mungu. Kupitia kifo, kuzikwa, na kufufuka kwa Yesu, Mungu amezishinda nguvu za shetani na kubatilisha athari za laana. Sasa, katika maisha yenyewe ya Kanisa, utawala wa Mungu upo na unaishi kwenye sayari ya dunia. Taswira hii ina umuhimu maalum kwa jamii za mijini, ambazo zinakabiliana hasa na aina hii ya vita vya kiroho vinavyoendelea. Jibu maswali yaliyo hapa chini kwa ufupi na kikamilifu, na uhakikishe kuwa unaelewa mawazo ya msingi yanayohusiana na taswira hii muhimu. 1. Kwa nini tunaweza kusema kwamba taswira ya Utume kama Vita vya Milki inaweza kuwa taswira ya utume na maisha ya kiroho ambayo ni unganishi na yenye nguvu zaidi katika Maandiko yote? Je, taswira hii inahusiana vipi na wazo la kuanzishwa na kutangazwa kwa utawala wa ufalme wa Mungu kuptia Yesu wa Nazareti? Eleza. 2. Toa maelezo mafupi ya taswira ya Mungu kama Shujaa wa kiungu katika Maandiko. Taswira hii inasisitiza nini kuhusu “siri ya kuasi”? Ni nini kilichotukia kama matokeo ya upinzani dhidi ya utawala wa Mungu mbinguni, na madhara yake kwa uumbaji yalikuwa nini? 3. Kwa nini protoevangelium ni muhimu sana kwa ajili ya kuelewa jukumu la Mungu na utambulisho wake kama Shujaa? (rej. Mwanzo 3:15). Je, ni kwa jinsi gani siri ya uovu, Anguko, na laana vilibadilisha kwa kina uhusiano wa Mungu na uumbaji wake, hasa na wanadamu? 4. Je, mapambano ya Mungu dhidi ya uovu yalidhihirishwa kwa vielelezo na njia zipi katika Agano la Kale? Je, mapambano ya Mungu dhidi ya Farao na mataifa ya Kanaani yanatusaidiaje kumwelewa Mungu kama Shujaa wa kiungu? Kwa nini Mungu pia alichukua nafasi ya Shujaa dhidi ya watu wake mwenyewe? 5. Manabii wa Israeli walionyesha jinsi gani kuja kwa Masihi kama muendelezo wa jukumu la Mungu kama Shujaa wa kiungu, na Masihi huyo angeharibuje uovu wote hatimaye mara moja, milele?

Sehemu ya 2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

2

Made with FlippingBook Annual report maker