https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 0 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

2. Amewapa watu wake mamlaka juu ya yule mwovu kwa kuwahamisha kutoka katika ufalme wa giza na kuwaingiza katika Ufalme wa Kristo (Kol. 1:13).

C. Utume ni udhihirisho na tangazo la utawala wa Mungu unaotenda kazi hapa na sasa .

1. Utume ni kutabiri ukombozi kwa wafungwa, Rum. 10:9-10.

2. Tumewekwa huru kutoka katika utumwa wa adui kwa njia ya Yesu Kristo, Ebr. 2:14-15; 1 Yohana 3:8; 1 Yohana 4:4.

2

3. Uasi wa Shetani umezimwa, lakini bado ana uwezo wa kudanganya na kutesa, 1 Pet. 5:8; Yakobo 4:7.

4. Adhabu yake ni ya hakika; hakuna kitu kinachoweza kuzuia kurejeshwa kikamilifu kwa mapenzi ya Mungu juu ya vitu vyote, Ufu. 11:15-18, taz. 15.

D. Kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi ni kuendeleza utawala wa Mungu kwa kushuhudia kuja kwake katika nafsi ya Yesu wa Nazareti!

Hitimisho

» Mojawapo ya taswira zenye kuvutia na zenye nguvu za utume katika Maandiko ni tangazo la utawala wa ufalme wa Mungu katika nafsi ya Yesu wa Nazareti. » Kupitia kifo, kuzikwa, na kufufuka kwa Yesu, Mungu amezishinda nguvu za shetani na kubatilisha athari za laana. Sasa, katika maisha yenyewe ya Kanisa, utawala wa Mungu upo na unaishi kwenye sayari ya dunia. » Hata hivyo, Ufalme bado haujakamilishwa kikamilifu na hautakamilishwa hadi Kristo atakapokuja tena.

Made with FlippingBook Annual report maker