https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 0 5

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

5. Damu ya Yesu Kristo na neno la ushuhuda wao, Ufu. 12:10-11. Utume sio kitu kingine bali ni kuingizwa kwa vikosi vya askari wa Mungu wa mashambulizi mazito kwenye eneo la adui shetani. Upinzani wa Shetani dhidi ya ushindi na mamlaka ya Kristo utakuwa na nguvu na ukatili; ni wale tu walioagizwa na Neno lake kuu na mamlaka ya ufalme wanaweza kusimama na kushindana siku ya uovu , Efe. 6:10-18.

F. Hivi karibuni, utawala wa Mungu utakamilika katika Enzi Ijayo wakati wa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, Rum. 16:20.

IV. Dondoo za mwisho za utume kama Vita vya Milki

2

A. Utawala wa Mungu juu ya ulimwengu wake sasa unathibitishwa tena katika Yesu Kristo.

1. Yesu wa Nazareti ndiye Masihi aliyetabiriwa, ambaye amepewa daraka la kurejesha utawala wa Mungu katika ulimwengu wote mzima, Yohana 1:41-45; Mt. 28:18.

2. Kama matokeo ya utii na kifo chake, ameinuliwa hadi mkono wa kuume wa Baba, kama Bwana juu ya yote, Flp. 2:9-11; Efe. 1:20-23; Flp. 3:20-21.

3. Kama Bwana wa wote, yeye ndiye Bwana wa mavuno (ya utume), na anawaongoza watu wake kwenye ushindi ulimwenguni pote wanapotangaza utukufu wake kwa mataifa, Mdo 1:8; Mt. 9:35-38; Mt. 28:18-20.

B. Mungu ni Shujaa ambaye mamlaka yake kupitia Masihi Yesu yamezishinda nguvu za shetani na mapepo waovu, na madhara ya laana.

1. Amewavua silaha na kuwaaibisha kwa njia ya msalaba, Kol. 2:15.

Made with FlippingBook Annual report maker