https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 1 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

* Ni kwa njia gani tunapaswa kufundisha historia ya Israeli kama historia yetu kwa ajili ya maelekezo, kujifunza, na kujengana? (Taz. 1 Kor. 10:6 11: Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. 10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani ). * Je, lugha ya Biblia kuhusu vita, migogoro, na mapambano inapatana na uzoefu wako mwenyewe kama mwamini? Je, tunapaswa kutumiaje lugha na taswira hizi katika maisha yetu wenyewe kama wanafunzi wa Yesu? * Je, kuna watu hasa ambao wewe binafsi usingependa waitikie Injili ya Bwana na kuokolewa? Ina maana gani kwako kwamba Mungu anaweza kumvuta yeyote amtakaye wakati wowote kutoka mahali popote ili awe sehemu ya mwili wake na bibi-arusi wake (rej. Yoh. 6:44)? * Je, unajiona kuwa askari-jeshi wa Yesu Kristo, na ikiwa sivyo, kwa nini? Ikiwa unajisikia vizuri na taswira hii, kwa nini hufikirii kuwa ni taswira maarufu zaidi na inakubalika katika makusanyiko yetu leo? Kwa lugha nyingine, unadhani ni kwa nini Wakristo wengi hawavutiwi sana na taswira hii ya kivita? * Je, ni jambo la busara kutumia taswira, mifano, na ishara za vita leo, ukizingatia mizozo yote inayoendelea ulimwenguni na wasiwasi ulioenea ulimwenguni pote kuhusu ugaidi? Je, tunapaswa kuacha kusisitiza taswira hizi ili tusieleweke vibaya na wengine leo? * Je, unaishi kama mtu unayeamini kwamba Ufalme wa Mungu umethibitishwa tena katika uwepo wa Yesu ndani ya Kanisa? Unaliona kanisa lako la mahali pamoja kama “ishara na kionjo cha Ufalme wa Mungu” duniani leo? Kama ndiyo au siyo eleza kwa nini. * Malizia sentensi ifuatayo: “Ikiwa kungekuwa na jambo moja tu ambalo ningeweza kufanya ili kufanya mambo haya yawe hai maishani mwangu sasa hivi, mahali nilipo, lingekuwa.......

2

Made with FlippingBook Annual report maker