https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 1 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

MIFANO

Taswira za Vita Hazijengi Imani

Ijapokuwa Biblia imejaa mafumbo, taswira, mifano, na muhtasari wa hekaya ya vita vya ulimwengu wa roho, Yahweh akiwa Shujaa, na Kristo akiwa Mshindi mkuu juu ya Shetani, kifo, laana, na nguvu za giza, Wakristo wengi wa sasa hawapendezwi na taswira hizo. Katika ulimwengu unaokumbwa na ugaidi, mizozo, na vita, Wakristo wengi wanyoofu hawaamini kwamba taswira na mitazamo ya aina hiyo ni muhimu. Badala ya kuelekeza kwenye moyo wa Injili, upendo wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kifo cha Yesu Kristo kwa ajili ya ulimwengu, taswira kama hizo za vita zinachanganya watu, zinaingiza mawazo ambayo ni magumu kueleweka ulimwenguni leo, na zinaweza hata kufifisha mtazamo wa jumla wa huruma ya Mungu kwa maskini na wanaokandamizwa. Wakristo wengine (ambao ni wanyoofu vile vile na wa kibiblia) wanahisi kwamba kupuuza au kujitenga na msisitizo wa kibiblia juu ya vita vya kiroho ni kujinyima fursa ya kupata ufahamu juu ya taswira ambayo pengine ndiyo yenye nguvu na muhimu zaidi iliyotolewa katika Maandiko kwa ajili ya kutuwezesha kuuelewa ulimwengu wa kiroho. Hawa wanaoona thamani ya taswira za vita wanathibitisha kwamba hatufanyi vita dhidi ya wanadamu, bali tunapigana dhidi ya nguvu ambazo zinatafuta kutuangamiza: “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Efe. 6:12). Taswira hizi zinatupatia ufahamu mkubwa katika ulimwengu wa mapambano ya Kikristo, ambayo ni vita kati ya wema na uovu, na tunapaswa kujifunza kupitia taswira hizi. Ni kundi lipi kati ya makundi haya mawili ambalo unadhani liko sahihi katika kuelezea asili ya imani ya Kikristo katika ulimwengu wa leo: je, tunapaswa kutafuta taswira nyingine ili kuelewa na kufafanua imani yetu katika ulimwengu huu ulioharibiwa na vita na migogoro, au tunapaswa kuzitumia taswira hizi hizi za Biblia za vita na mapambano ili wengine waweze kuelewa vyema zaidi asili ya vita ni nini hasa, na ni muhimu kiasi gani kwao kuelewa na kutumia taswira na picha hizi katika maisha yao? (Inatokana na kisa cha kweli). Dada wawili wamishenari, wote wasioolewa, waliojitoa kwa dhati kwa Mungu, na ambao ni wanafunzi waaminifu wa Kristo, walitoa maoni yao kuhusu aina za taswira na mada zinazosisitizwa leo katika Kanisa. Wote wawili wanaamini kwamba mkazo juu ya Mungu kama Hakimu, Mfalme, na Muumbaji ni wa kawaida sana na hauna mguso wa kuweza kuathiri mazingira ya kisasa ya mijini. Kwa maoni yao, wazo la taswira ya ndani zaidi, ya kibinafsi, na ya upendo kuhusu Yesu kama bwana-arusi linatoa tumaini bora zaidi la kuweza kuwaonyesha watu moyo wa Mungu kwa ukamilifu zaidi na katika Je, ni Ubinafsishaji Mbaya wa Taswira ya Ndoa?

1

2

2

Made with FlippingBook Annual report maker