https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 1 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
muktadha bora, sahihi na wenye mguso zaidi leo. Wote wawili walionyesha uelewa wao wa taswira ya ndoa kwa njia ya ukaribu zaidi, hata kufikia kuwa ya hatari na yenye hatihati ya kuwa ya kimahaba kidogo na hata isiyofaa. Ingawa walifahamu kuhusu mwelekeo wa mtazamo wao, walikataa mahusia yoyote kwamba taswira hii haifai kuchukuliwa kibinafsi kwa ajili yao kama waseja. Kimsingi taswira hii imekuwa msingi wa hoja nyingi za kawaida za Kikristo kuhusu useja kwa akina dada wanaojisalimisha kwa Kristo kwa ajili ya kumtumikia bila kuolewa wakijiaminisha kwamba wameolewa na Kristo. Ungewajibuje dada hawa wawili wapendwa wamishenari kuhusiana na suala hili? Je, kubinafsishwa kwa taswira hii kiasi hiki kunafaa, au je, tunapaswa kuitumia tu kuzungumzia watu wote wa Mungu kwa ujumla kama bibi-arusi wa Kristo, na si watu binafsi wanaoiona kuwa muhimu kwa maisha yao ya kibinafsi? Kuhusiana na taswira ya vita katika suala la ufuasi wa Kikristo na utume, mtu anaweza kuona tofauti kubwa kati ya hali ya kiroho na mapambano ya mijini na ile ya maeneo ya kando kando mwa miji. Tukizungumza kwa ujumla, kwa wakazi wengi wa vitongoji ambao wamepata kiasi fulani cha utajiri na urahisi wa maisha, mkazo mkubwa katika safari yao ya kiroho ni usalama na ulinzi. Mara nyingi katika maeneo kama hayo, jamii inachukuliwa kama ni nguvu ovu inayopambana kutaka kuharibu maadili mema na heshima ya familia. Hivyo lengo linakuwa kuhifadhi maadili haya mema na mifumo ya imani ili kuhakikisha kwamba familia na mitaa inawekwa katika usalama kutokana na nguvu ambazo zingejaribu kudhoofisha usalama huo. Kwa upande mwingine, hali ya kiroho katika maeneo ya mijini inaelekea kusisitiza zaidi mzozo na mapambano dhidi ya mifumo ya ulimwengu na mawakala wake. Vita vinakumbatiwa kama jibu na suluhisho la lazima dhidi ya uovu uliopo kila mahali unaotaka kuwaharibu na kuwaangamiza watu. Mwelekeo wa Mkristo mkomavu anayeishi mjini utakuwa wa kujitahidi kuwa macho na mwenye umakini wakati wote na kukabiliana mara kwa mara na mamlaka za giza, kujitahidi kushinda nguvu hizi kila siku. Mawazo yake hayawi katika kuhifadhi maadili, bali ni kuwakomboa watu kutoka katika mifumo dhalimu na hatari inayowashikilia. Wengi wao hawana chochote cha kulinda wala utajiri wa kuhifadhi, bali wana mwelekeo wa kukumbatia mitazamo ya kiroho ambayo inasisitiza vita na mapambano. Je, una maoni gani kuhusu mitindo hii tofauti ya kiroho – je, ni matokeo tu ya safari za maisha ya kiroho kulingana na mazingira tofauti, au kuna jambo la msingi zaidi katika dhana hizi tofauti na utendaji wake katika maisha ya kiroho? 3 Hali ya Kiroho katika Vitongoji na Hali ya Kiroho ndani ya Miji
2
Made with FlippingBook Annual report maker