https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 1 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Je, Ukristo ni Dini ya Magharibi?
Kwa bahati mbaya, wengi wamehusisha kimakosa imani nzima ya Kikristo na aina fulani ya udhibiti wa mfumo wa utamaduni wa Ulaya ambao unafanya Ukristo uonekane kama imani ya watu wa Magharibi, weupe, wa tabaka la kati. Japokuwa vuguvugu lenye nguvu na kasi zaidi la Kikristo kwa sasa linapatikana katika ulimwengu wa tatu na linahusisha watu wa rangi tofauti na nyeupe, bado ni ukweli dhahiri kwamba taasisi zenye nguvu na fedha kwa sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kikristo bado ni za watu weupe, wa nchi za Magharibi. Seminari nyingi na vyuo vya Kikristo, taasisi za uchapishaji, na madhehebu ya kikanisa pamoja na mashirika ya Kikristo yanaendeshwa na watu kwa asilimia kubwa wa Ulaya au Amerika Kaskazini, kwa kawaida wazungu, wenye mahusiano na watu wenye mamlaka na rasilimali muhimu. Kwa sababu hiyo, watu wengi kutoka nje, hawauoni Ukristo kama “watu wapya wa Mungu” waliojengwa juu ya misingi ya usawa, kuchangamana, utofauti, na umoja wa mataifa mbalimbali na tamaduni nyingi, wakifurahia kifungo kimoja cha upendo katika Roho. Badala yake, mwili wa Kristo na bibi-arusi wa Kristo (Kanisa) anaonekana kama “watu wa Mataifa” katika mwelekeo wao, na wa magharibi katika utawala wao. Mawazo haya yanadhoofisha uwezo wetu wa kuingia katika jamii fulani ambazo zinauona Ukristo kama dini ya kimagharibi na ya kitamaduni; mataifa mengi hayako wazi tena kupokea wamishenari wa Kikristo, wakiwaona kama mawakala wa maadili na kanuni za kimagharibi, na si wawakilishi wa raia wa mbinguni. Kutokana na uadui unaozidi kuongezeka dhidi ya Ukristo na u-Magharibi, je, sisi kama viongozi wa umisheni tunapaswa kufikiria vipi kuhusu kizazi kijacho cha kumpeleka Kristo katika tamaduni mbalimbali, hasa zile ambazo zina hofu na zinatilia shaka chochote cha magharibi na cha “kizungu”? Mapenzi ya kiungu kati ya Mungu na watu wake ni mojawapo ya sababu kuu za utume katika Maandiko Matakatifu, yaani, azimio la Mungu la kuvuta watu kutoka ulimwenguni ili wawe milki yake mwenyewe, milki iliyotimizwa na kukamilishwa katika upendo wa Yesu kwa Kanisa lake. Wazo la bwana-arusi na bibi-arusi katika Agano la Kale linajulikana sana, linahusishwa kwa ukaribu na wazo la muungano wa kijamii, furaha, na shangwe katika Maandiko, pia linatumika kama taswira ya msingi ya uhusiano wa Mungu na watu wake (kama inavyoonekana katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora). Hatimaye, watu wa Mungu wangerejeshwa kwake, na Yeye angecheza na kushangilia juu ya watu wake kama bwana-arusi afanyavyo juu ya bibi-arusi wake. Vidokezo vya tumaini na ahadi ya agano jipya vimejumuishwa katika agano la Mungu na Ibrahamu, na matarajio yake ya kujumuishwa kwa Wasio Wayahudi. Katika Yesu Kristo, taswira ya bwana-arusi imepanuliwa na
4
2
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook Annual report maker