https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 2 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
ya ufafanuzi wa Maandiko. Kadiri unavyochagua mapema, ndivyo utakavyokuwa na muda mwingi wa kujiandaa!
Katika somo hili tulichunguza taswira mbili: mapenzi ya kiungu na Vita vya Milki , na tukazingatia maana yake katika kuelewa jukumu la umisheni wa Kanisa leo. Tuliona jinsi kusudio la Mungu la kuvuta kutoka duniani kote watu ili waweze kuwa milki yake mwenyewe lilitia ndani hata watu wa Mataifa, ambao sasa kwa imani wanaweza kushiriki katika mpango mzuri ajabu wa Mungu wa kuumba watu watakaoishi pamoja naye milele. Pia tuliona jinsi Mungu anavyoimarisha utawala wake wa ufalme kupitia Yesu wa Nazareti, ambaye kwa kifo chake, kuzikwa, na ufufuo wake alishinda nguvu za ibilisi na kubatilisha madhara ya laana. Sasa, katika maisha yenyewe ya Kanisa, utawala wa Mungu upo na unaishi kwenye sayari ya dunia. Katika somo letu linalofuata tutaangalia zaidi vipengele vya msingi wa utume wa Kikristo, tukizingatia moja ya vitu vyake muhimu zaidi vya kuzingatia: jiji. Tutazingatia umuhimu wa kiroho wa jiji, na namna Mungu alivyolichukua wazo la jiji na kulifanya kuwa ishara ya makusudi yake mwenyewe, akilibadilisha kutoka sura ya uasi na ibada ya sanamu hadi makao yake yaliyo juu. Kwa kuzingatia ufahamu huu, tutachunguza sababu tatu muhimu kwa nini umisheni wa mijini ni muhimu kwetu leo. Mji kama makao ya ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho ulimwenguni, unakuwa sumaku inayowavuta watu wengi waliokandamizwa, waliovunjika moyo na maskini, na unaonekana kama picha ya hatima na urithi wetu wa kiroho. Sababu hizi tatu zinazaa wito wa kibiblia wenye nguvu kwetu kufanya yote tuwezayo kutangaza Injili, kufuasa, na kupanda makanisa katika miji yetu, nyumbani na nje ya nchi.
Kuelekea Somo Linalofuata
2
Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .
Made with FlippingBook Annual report maker