https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 1 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

pamoja na Mungu katika pambano kubwa zaidi, endelevu la muda mrefu. Ushindi wa imani wa Yakobo haungeweza kupatikana bila pambano lile la usiku kucha. Ujuzi wa kina wa Mungu hauwezi kufikiwa kupitia mazungumzo mafupi kama ya simu za dharura. Mungu hatoi vipawa vyake kwa waombaji wa mazoea wa kuingia na kutoka au wenye haraka. Muda mwingi na Mungu pekee ndiyo siri ya kumjua na kuwa na ushawishi naye. Anafurahia pale mtu anayemjua anapoendelea kung’ang’ania kwa imani. Yeye huwapa karama zake kuu sana wale wanaotangaza hamu yao ya kuzipokea na kuzithamini karama hizo kwa uthabiti pamoja na bidii na uimara wao. Kristo, ambaye katika hili na mambo mengine ni Mfano wetu, alikesha usiku mara nyingi katika maombi. Kawaida yake ilikuwa kuomba sana. Alikuwa na mahali pake pa kawaida pa kuomba. Historia yake na tabia yake vilijaa misimu mingi mirefu ya kuomba. Paulo aliomba mchana na usiku. Ilimgharimu Danieli kuacha mambo muhimu sana kwake ili kupata muda wa kuomba mara tatu kwa siku. Maombi ya Daudi ya asubuhi, adhuhuri, na usiku bila shaka katika vipindi vingi yalikuwa ya muda mrefu sana. Ingawa hatuna simulizi mahususi kuhusu muda ambao watakatifu hao wa Biblia walitumia katika maombi, lakini dalili zinaonyesha kwamba walitumia muda mwingi katika maombi, na nyakati fulani walikuwa na desturi ya kuwa na misimu mirefu ya maombi. ~ E. M. Bounds. Power Through Prayer . (toleo la kielektroniki). Oak Harbor, WA: Logos Research Systems, 1999. Weka dhamira, katika kipindi chote cha kujifunza kozi hii, kwamba utaomba kwa muda mrefu juu ya moyo wako mwenyewe, mahitaji ya wanafunzi wenzako, na maombi ya wazi kwa Bwana kuhusu uongozi wake na kweli hizi maishani mwako.

2

MAZOEZI

Waefeso 5:25-27 na Waefeso 6:10-13

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya usomjai ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.

Kazi ya Usomaji

Tafadhali soma kwa umakini kazi zilizo hapo juu, na kama wiki iliyopita, ziandikie muhtasari mfupi na ulete muhtasari huo darasani wiki ijayo (tafadhali tazama “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Pia, sasa ni wakati wa kuanza kufikiria kuhusu aina ya kazi yako ya huduma kwa vitendo, na pia kuamua ni kifungu gani cha Maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi yako ya ufafanuzi wa Maandiko. Usichelewe kufanya maamuzi kuhusu kazi yako ya huduma au ile

Kazi Nyingine

Made with FlippingBook Annual report maker