https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 1 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Ikiwa ungependa kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo ya somo hili la Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Pili , unaweza kutaka kujaribu vitabu hivi: Costas, Orlando E. Christ Outside the Gate: Mission Beyond Christendom. Maryknoll, NY: Orbis Books, 1982. Curtis, Brent, and John Eldredge. The Sacred Romance: Drawing Closer to the Heart of God. Nashville: Nelson Books, 1997. Jones, E. Stanley. Is the Kingdom of God Realism? New York: Abingdon Cokesbury, 1940. Newbigin, Lesslie. Sign of the Kingdom. Grand Rapids: Eerdmans, 1980. Yoder, John Howard. The Politics of Jesus. Grand Rapids: Eerdmans, 1972. Mwombe Mungu Roho Mtakatifu akusaidie kutafakari juu ya mada zinazozungumziwa katika somo hili ili upate njia za kuhusianisha kweli za somo hili na fursa za vitendo katika maisha na huduma yako mwenyewe. Chagua mada moja au zaidi, muhimu, na mawazo ya kufikiria na kuombea katika wiki hii yote ijayo, na uwe wazi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu kuhusu njia mahususi unazoweza kuelewa vyema na kutumia maana za mada hizi katika mafundisho yako, mahubiri, na ushuhudiaji. Mtafute Bwana pamoja na wanafunzi wenzako katika kuombeana na kuombea mambo ambayo Mungu amefunua katika somo hili. Pia, weka ahadi ya kutumia muda mrefu wa maombi pamoja na Bwana, peke yako na ikiwezekana pamoja na wengine katika wiki. Muda mrefu wa maombi ni muhimu sana kwa ajili ya kukuwezesha kutumia kweli za mafundisho na kuleta mabadiliko ya maisha mbele za Bwana. Mwandishi E. M. Bounds anaweka jambo hili wazi: Ingawa maombi mengi ya faragha, katika hali ya kawaida, lazima yawe mafupi, na pia maombi ya hadhara, kama kanuni, yanapaswa kuwa mafupi na yenye kiasi; kukiwepo na nafasi ya kutosha kwa ajili ya maombi mafupi mafupi, na ingawa maombi mafupi yana thamani – bado katika ushirika wetu wa faragha na Mungu muda ni kipengele muhimu kinachoamua thamani ya mambi yetu. Kutumia muda mwingi na Mungu ndiyo siri ya maombi yote yenye mafanikio. Maombi ambayo yanaonekana kama nguvu kuu ni matokeo ya moja kwa moja ya muda mwingi unaotumiwa mbele za Mungu. Maombi yetu mafupi yanakuwa na mantiki na ufanisi kwa sababu ya yale marefu yaliyotangulia. Maombi mafupi yenye nguvu na ushindi hayawezi kufanywa na mtu ambaye hajashinda

Nyenzo na Bibliografia

2

Kuhusianisha Somo na Huduma

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook Annual report maker