https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 2 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Utume wa Kikristo na Jiji

SOMO LA 3

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kufafanua dhana ya jiji kwa mujibu wa Biblia, ikijumuisha ukweli kwamba miji ilikuwa mikusanyiko ya nyumba na majengo yaliyozungukwa na kuta, ilikuwa muhimu na ya kuvutia kwa wakati wao, na kwamba baadhi ya miji ilitegemea miji mingine kwa ajili ya kupata ulinzi na mahitaji muhimu. Miji, iliyozoeleka katika ulimwengu wa kale ilikuwa midogo, kwa kawaida isiyo na lami, iliyoimarishwa na kuta nene na minara mirefu, na ilitumika kama makao ya serikali na mamlaka. • Kufafanua maana ya kiroho ya mji, yaani, njia ambazo miji ilihusishwa na uasi wa kibinadamu na ibada ya sanamu (Henoko, mji wa Kaini), na uhuru na kiburi (kama ilivyokuwa kwenye Mnara wa Babeli), na uovu na kutomcha Mungu (kama vile Babeli). Miji ilihukumiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zake (k.m. Sodoma na Gomora, Yeriko, Ninawi), na kushutumiwa kwa kujidhania kwa uongo kwamba ina usalama na uwezo (hasa, Yerusalemu). • Kuonyesha jinsi Mungu alivyokubali mji kuwa ishara ya makao yake na baraka zake, yaani, kuichagua Yerusalemu kwa ajili yake mwenyewe, na azimio lake la kuifanya kuwa sifa duniani. Kuonyesha zaidi tendo la Mungu kugeuza taswira ya uasi kuwa taswira ya kimbilio (k.m, miji ya makimbilio), pamoja na taswira ya mahali ambapo watu wanaweza kuujua na kuupokea msamaha na baraka zake (k.m. Yona na suala la mji wa Ninawi). • Kueleza jinsi ambavyo, kwa sababu ya rehema na fadhili za Mungu mwenyewe, kunaweza kuwa na tumaini kwa mji wowote unaotubu mbele ya hukumu yake, unaojinyenyekeza chini ya matakwa yake, na kutafuta rehema zake mbele ya adhabu yake. • Kutoa ushahidi wa sababu tatu muhimu kwa nini umisheni katika miji lazima uwe kipaumbele cha shughuli zote za umisheni leo. Haya ni pamoja na yafuatayo: miji ni vituo vya ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho katika ulimwengu, ni sumaku inayovuta watu wengi waliokandamizwa,

Malengo ya Somo

3

Made with FlippingBook Annual report maker