https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 2 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

waliovunjika moyo, na maskini, lakini pia miji ni taswira ya hatima yetu na urithi wetu wa kiroho. • Kuonyesha jinsi huduma ya Yesu mwenyewe ilivyokuwa na msingi wake katika miji, na agizo lake la kutangaza Injili lilitia ndani kuhubiri Ufalme kuanzia Yerusalemu; pia, jinsi Ukristo ulivyozaliwa katika mji, na kuenea katika himaya ya Kirumi katika karne ya kwanza kupitia vituo vikuu vya miji vya wakati ule (katika sehemu kama vile Dameski, Antiokia, Korintho, Filipi, Thesalonike, Athene, na Roma yenyewe). Huduma ya kitume (pamoja na safari za Paulo) kimsingi zilikuwa za mijini, vituo ambavyo vilikuwa kama malango ya himaya pana ya Kirumi. • Kutoa muhtasari wa ukubwa, upeo, na idadi ya watu wa baadhi ya majiji leo. Zaidi ya hayo, kuonyesha jinsi majiji hayo yanavyotumika kuwa makao ya serikali, elimu, afya, habari, burudani, biashara, uchumi, viwanda, sheria, jeshi, na dini. Kuorodhesha miji kulingana na umuhimu wake kama miji ya kitamaduni (ambayo inaongoza ulimwengu kwa mitindo ya mavazi, mienendo na maoni), miji ya kisiasa na kiutawala (vituo vya vyombo vya maamuzi ulimwenguni kote, au vituo vya mamlaka za kiserikali na urasimu wake), miji ya viwanda (miji yenye kelele na shughuli nyingi za uzalishaji wa viwandani) miji ya kibiashara (masoko na maduka makubwa ambapo bidhaa na huduma hubadilishwa kwa kiwango cha kimataifa), miji ya alama au ya kihistoria (miji ambayo mapambano makubwa ya kihistoria yanapiganwa, kutatuliwa, na kuwekewa alama za kumbukumbu), na miji ya msingi (ambayo inachanganya sifa zote pamoja). • Kuonyesha njia ambazo miji leo inatumika kama sumaku ya kuwavuta waliodhulumiwa, waliovunjika moyo, na maskini, ikijumuisha mwelekeo wa kibiblia juu ya moyo wa Mungu kwa ajili ya watu maskini, mwelekeo wa ukuaji wa miji (na mlundikano wa makundi ya watu maskini ndani yake) kama sifa kuu ya hali ya miji ya nyakati za sasa, na hoja ya kimantiki kwamba ikiwa Mungu anawajali maskini, basi lazima vile vile anajali kuhusu miji na majiji ya Marekani na kwingineko duniani kwa sababu ya idadi kubwa ya watu maskini wanaoishi katika miji na majiji hayo. • Kufanya muhtasari wa data muhimu za kibiblia kuhusu jinsi jiji lilivyo picha na ishara ya hatima yetu na urithi wetu wa kiroho, kwa maana ya tumaini la Yerusalemu Mpya; huu hautakuwa mji ambamo Mungu hayumo na ambamo kiburi kinatawala, bali utakuwa mji ambamo Mungu atakaa, na Yesu ataabudiwa kama Bwana wa wote. Kuonyesha jinsi ambavyo lengo la wazi la utume ni kuvuna miji ya ulimwengu ili kujaza Yerusalemu Mpya,

3

Made with FlippingBook Annual report maker