https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 2 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
mama wa kweli wa waamini wote (mradi wa mwisho wa ukarabati wa miji). • Kuelezea mambo muhimu katika kuelewa umuhimu mkubwa wa miji na majiji kwa ajili ya utume wa mijini, yaani kwamba katika mikakati na shughuli zote za utume wetu wote – kuomba, kutoa na kutuma – tunapaswa kuzingatia umuhimu wa miji. Lazima tuajiri wafanyakazi wa kiroho zaidi ili kuhudumu katika miji na majiji, kupanga mikakati ya jinsi ya kuifikia miji ambayo haijafikiwa na Injili, na kuomba kwa ajili ya miji na majiji na kutafuta usalama wake, tukitambua kwamba miji na majiji yakiwa na usalama, basi na sisi tutapata hifadhi na usalama ndani yake. Waebrania 11:8-16 – Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. 11 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. 12 Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika. 13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. 14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. 16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. “Jumba kuu la imani” linalozungumziwa hapa linawakilisha moja ya vilele vya Agano Jipya, na linazungumzia umoja na muunganiko wa ajabu ambao waamini wote wanao baina yao kupitia imani yao katika Kristo. Kwa maana halisi, waamini wote wa kila zama na nyakati wameunganishwa katika mkanda mmoja usio na mshono – mkanda wa matumaini na imani, wa upendo kwa Mungu na upendo kati yao, wa matazamio halisi na ya kweli ya utimilifu wa ahadi ya Mungu kwa kila mmoja kibinafsi na kwa wote kwa pamoja. Hapa, katika kifungu hiki cha Waebrania 11, tunaona kwamba tumaini limefafanuliwa kwa maana ya nchi iliyo bora zaidi, nchi ya mbinguni ambayo inahusisha ushirika na Mungu bila kutahayarika, na makao katika mji ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu mwenyewe. Mungu Ametuandalia Mji
Ibada
3
Made with FlippingBook Annual report maker