https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 2 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Je! hilo linakushangaza—kwamba Mungu anaandaa jiji kwa ajili ya watakatifu wa nyakati zote? Kwa Wakristo wengi leo, wazo la jiji linawapa taswira ya kutisha, ya kuogofya, na isiyopendeza. Wazo la jiji linawapa picha yenye utata wa ajabu, msongamano, uchafuzi wa mazingira, na kelele, vikihusianishwa na shughuli nyingi mno, msongamano wa watu na vyombo vya usafiri, uhalifu na jeuri, na ukosefu wa maadili. Ni kwa jinsi gani (au hata kwa nini ) Mungu angetaka kujenga jiji kwa ajili ya wanadamu kuishi milele, na kwa nini hili liwe jambo muhimu katika tumaini la msingi la watakatifu wote, katika vizazi vyote? Maswali mazuri, lakini kwa kweli, Biblia imetoa majibu bora zaidi! Kwanza kabisa, wazo la kwamba Mungu anaandaa mahali kwa ajili ya walio wake ni mada ya kawaida na inayopendwa sana katika Biblia, ambayo imeangaziwa na kutajwa mara nyingi katika Agano Jipya. Katika hukumu ya kondoo na mbuzi, Yesu anatangaza kwamba mfalme atawaambia wale walio katika haki yake waje na kuurithi Ufalme ulioandaliwa na Baba kwa ajili yao tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu (Mt. 25:34). Yesu aliwafariji wanafunzi wake kwa kuwaamuru wasiogope, kwa kuwa ilikuwa ni furaha ya Baba kuwapa Ufalme (Lk. 12:32), na aliahidi kwa uhakika kwamba nyumba ya Baba yake inayo makao mengi, na kwamba anaenda kuandaa mahali kwa ajili yao ili wakae pamoja naye milele (Yoh. 14:1-4). Paulo anawaambia Wafilipi kwamba uraia wa waaminio uko mbinguni, na ni kutoka huko tunamngojea Mwokozi, Bwana Yesu Kristo ambaye atabadilisha miili yetu dhaifu ipate kufanana na mwili wake wa tukufu wake, kwa uwezo alionao sasa wa kuvitiisha vitu vyote chini ya mapenzi yake (Flp. 3:20-21). Kwa kweli, maono ya tumaini la Kikristo ni wazo la maandalizi ambayo Mungu anafanya ya makao kwa wale ambao wanarithi wokovu wake, na katika hali ya kushangaza, maono hayo yanaelezewa kuwa ni jiji. Zaidi ya hayo, hakuna Mkristo anayeweza kusoma maelezo kuhusu Yerusalemu Mpya halafu akakosa kustaajabishwa nayo na kujawa na tumaini na matarajio. Mji unaometa wa dhahabu safi, unaokaliwa na Baba na Mwana, usio na haja ya nuru kwa vile utukufu wa Bwana mwenyewe huuangazia. Ni nani awezaye kuuelezea uzuri wa mji ambao kazi zake za ndani zilibuniwa na kuundwa na Mungu mwenyewe, ambao hauna makaburi wala chumba cha kuhifadhia maiti (kwa sababu hakuna wafu), hakuna hospitali wala duka la dawa (kwa kuwa hakuna magonjwa), hakuna mahakama wala gereza (maana hakuna uhalifu), na hakuna daktari wa akili wala mshauri nasaha (kwa sababu hakuna huzuni)? Vipimo vya jiji lenyewe vinaufanya kuwa zaidi ya mahali tu pa kawaida, ni jiji kama mwezi (maili 1500 mraba, ikiwa tunachukulia vipimo vya Yohana kihalisi), jiji lililobuniwa na kujengwa kwa mkono wa Mkandarasi wa Ulimwengu, Bwana wetu Yesu. Kama mwanatheolojia, ukweli hauniepuki kwamba Bwana wetu kwa maana ya kazi yake, alikuwa fundi seremala, na hakuwezi kuwa na shaka hata kidogo kwamba mji

3

Made with FlippingBook Annual report maker