https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 2 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
uliobuniwa na kujengwa na yeye utakuwa wa kuvutia kupita maelezo, na wa ajabu kupita fikra. Hata hivyo, licha ya baraka hizi zote za ajabu za jiji lenyewe, ajabu yake kuu ni kwamba makao ya Mungu sasa ni pamja na wanadamu: Ufu. 21:1-4 – Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita . Kinachoufanya mji huo kuwa wa kutamanika zaidi, wenye utukufu zaidi, na wa kushangaza zaidi ni kwamba ndani yake Mungu atakaa pamoja na wanadamu, naye atakuwa Mungu wao, nao watukuwa watu wake. Machozi yote yatafutwa, kifo kitaondolewa, vile vile kilio na uchungu, na ukatili wote wa zamani wa enzi za uasi wa kibinadamu vitaondolewa milele. Je, kuna kitu kweli kinaweza kuwa cha kustaajabisha na kuhitajika zaidi kuliko hiki? Ukweli kwamba jiji hapo awali lilikuwa mahali pa uasi na ibada ya sanamu unaifanya Yerusalemu Mpya kuwa ukweli wa ajabu na wa kushangaza zaidi. Ni nani ambaye angefikiri kwamba Mungu wa mbinguni angekubali wazo la jiji ambalo taswira yake ni uovu na kuligeuza kuwa picha na sura halisi ya paradiso yenyewe? Hekima na maarifa ya Mungu wetu hayachunguziki na yanapita fahamu zetu (taz. Rum. 11:34-)! Daima chukua muda kutafakari ukweli kwamba mwisho wa vitu vyote kwa wanadamu ni mji – ndiyo! Mji uliobuniwa na kujengwa na Mungu na uliotajirishwa sana na uwepo wake mwenyewe, lakini bado ni mji. Tumaini la watakatifu wa nyakati zote ni kukaa katika mji wa Mungu: Ebr. 11:10 – Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. Ebr. 13:14 – Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. Seremala wa Kiungu anamalizia kazi yake kuu ya kujenga mji kwa ajili ya watu wake kukaa milele. Kuna kitu chochote kizuri kusikia na cha ajabu zaidi ya hicho? Je,
3
Made with FlippingBook Annual report maker