https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 2 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
kuna yeyote aliye na akili ya ubunifu na mkono wa ufundi unaoweza kunyoosha, kuremba, na kukamilisha kazi kwa ubora kuliko yeye? Yule anayejivunia ubunifu wake wa kiwango cha kutisha alipoumba waridi au msonobari, je, tushindwe kumwamini kwamba ataifanya vizuri na kwa ubora zaidi kazi ya ajabu ya kutujengea mahali, kwa ajili yetu? Hebu na tufanye kazi mjini leo tunapoutafuta mji ujao, ambao mbunifu na mjenzi wake ni Mungu. Naam, Mungu anatuandalia mji. Baada ya kukiri na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyopo kwenye viambatisho), omba maombi yafuatayo: Ee Bwana, muumba wetu, kwa kinywa cha nabii wako mtakatifu uliwafundisha watu wako wa kale kuitakia amani miji walimokuwa wakiishi. Tunakabidhi mitaa yetu chini ya ulinzi na uangalizi wako, ili iepushwe na migogoro ya kijamii na uharibifu. Utupe nguvu ya kuishi kwa kusudi na kujali wengine, ili tuweze kuishi kama jamii ya haki na amani ambamo mapenzi yako yatafanyika; kwa njia ya Mwanao, Yesu Kristo Bwana wetu. Amina. ~ Presbyterian Church (U.S.A.) na Cumberland Presbyterian Church. Kitengo cha Huduma ya Theolojia na Ibada. Kitabu cha Ibada ya Pamoja . Louisville, KY: Westminister/John Knox Press, 1993. uk. 821.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
3
Weka kando daftari lako na nyenzo za kujifunzia, kusanya pamoja mawazo yako, kisha ufanye Jaribio la Somo la 2, Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Pili.
Jaribio
Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita: Waefeso 5:25-27 na Waefeso 6:10-13.
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
Made with FlippingBook Annual report maker