https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 2 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

MIFANO YA REJEA

Usasishaji wa Miji, Mtindo wa Yesu

Mwanafunzi yeyote wa kozi ya usasishaji (yaani uboreshaji) wa miji nchini Marekani anajua kwamba mabilioni ya dola yameingizwa katika miradi ya usasishaji wa miji katika jamii za mijini kote nchini. Tangu mwishoni mwa miaka ya 60, kiasi cha ajabu cha rasilimali, fedha, na juhudi kimeingizwa katika kufanya miji ya Marekani kuwa salama, yenye afya na mahali pafaapo zaidi pa kuishi na kulea familia. Licha ya kiasi hiki cha ajabu cha uwekezaji wa serikali na wa kiuchumi, miji yetu bado inakabiliwa na matatizo ya madawa ya kulevya, vurugu, familia zilizovunjika, na ukosefu wa haki za kiuchumi. Vikundi mbalimbali vya Kikristo vimeibuka na mikakati ya namna ya kuboresha na kufanya upya miji kwa kuzingatia zaidi kanuni za Kikristo za haki na amani. Wengine wanahamasisha kwamba watu binafsi na familia za Kikristo zihamishe makazi yao na kurudi kuishi katika jamii za mijini, wakitaka kuchochea mtazamo wa kibiblia zaidi kuhusu miji. Wengine wanajielekeza katika mikakati inayosisitiza zaidi utii wa sheria, kuwafanya wakuu wa familia kuwajibika zaidi, na kutia moyo tabia ya wale wanaotafuta kuinua maisha yao ili yawe bora kama ya wengine katika jamii kupitia elimu, bidii, na nidhamu. Kwa kuzingatia wito wa Wakristo kutenda haki na kazi ya kufanya wanafunzi wa Kristo katika jiji, ni aina gani ya mikakati unayoamini ni muhimu zaidi kwa huduma ya mjini yenye ufanisi na yenye mafanikio? Wakristo wengi leo ambao wanaamini sana katika ulinzi na afya ya familia ya nyuklia wana hakika kwamba mazingira ya maisha ya mijini yanaharibu ustawi wa familia na ustawi wa kiroho. Katika jamii zenye giza sana kiroho na ambazo zimehatarishwa na jeuri za magenge, dawa za kulevya, shule duni, mifumo duni ya kijamii, na hali duni ya kiuchumi, Wakristo fulani wamekuwa na maoni kwamba kuhama jiji ni njia pekee ya usalama na ustawi wa familia ya Kikristo. Wamehitimisha kwamba kwa sababu hizi na nyinginezo, maisha ya jiji ni sumu kwa familia ya Kikristo; wale wanaoweza kuzikimbia lazima wafanye hivyo ili kujilinda wenyewe dhidi ya ushawishi usio na maadili uliokithiri katika miji mikubwa. Licha ya msimamo wa baadhi ya Wakristo wanafunzi wa Yesu wenye nia ya dhati ya kukaa jijini ili kufanyika chumvi na nuru ndani yake, Wakristo wengi na makanisa yao wamehama na kujitenga mbali na jiji, na kuacha ombwe la kimaadili na kiroho ambalo ni vigumu kuliziba. Wengine wamekata tamaa kabisa, wakisema kwamba majiji ya kisasa ya Marekani ni makubwa sana na ni hatari mno kiasi kwamba hayawezi kukombolewa. Wanasisitiza kwamba si mahali pa kulea familia; kama haupo jijini, usiende kuishi huko. Wanadai “njia bora ya kusaidia maeneo ya mijini Familia Lazima Zikimbie Mfumo wa Maisha ya Jiji Ikiwa Zinataka Kustawi

1

3

2

Made with FlippingBook Annual report maker