https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 3 0 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

yaliokithiri kwa umaskini, ukatili na kila aina ya uovu sio kwenda au kuendelea kuishi katika maeneo hayo, maana kufanya hivyo ni kuyaongezea shida – bora kuondoka humo na kuhamia maeneo ya pembezoni ambayo ni salama zaidi.” Wakristo wenye msimamo wa aina hii wanasisitiza kwamba mkakati unaofaa wa kuleta mabadiliko mijini ni familia za Kikristo kutafuta njia mbadala na kuhama nje ya miji. Je, jibu lako ni lipi kwa aina hii ya mitazamo inayojengwa juu ya “hali halisi” (na wakati mwingine inayotokana na kukata tamaa) kuhusu majiji na athari zake kwa familia leo? Kuna mapokeo mazuri ya kisasa ya kibiblia ambayo yanasisitiza kwamba uhusiano muhimu zaidi kati ya Wakristo makini na miji ya kisasa ni uhusiano wa kinabii na wa matamko, yaani, kupiga kelele dhidi ya ukosefu wa haki, ukatili, uharibifu, na ibada ya sanamu katika majiji ya kisasa. Kwa kweli mapokeo haya yanajengwa juu ya mifano mingi ya kibiblia ya manabii waliopewa mzigo wa kupiga kelele dhidi ya dhambi za miji ya wakati wao: Isaya kwa jiji la Yerusalemu, Hosea kwa mji wa Samaria, na Yona kwa mji wa Ninawi (na wengine wengi). Wale wanaoshikilia mtazamo huu wanaona kwamba kiburi, uwezo, na hisia ya utoshelevu wa miji ya kisasa vinadhihirisha kwamba njia pekee ya kuwezesha jiji kujiona jinsi lilivyo, yaani kutambua dhambi na uovu wake, ni kupitia makabiliano ya kinabii, matangazo ya moja kwa moja ya Neno la kweli dhidi ya viti vya mamlaka kuhusu hitaji lao la kutubu na kubadilika kwa kufuata matakwa ya Mungu ya haki na uadilifu katika jiji. Je, unafikiri kwamba mkakati kama huo unaweza kuwa na ufanisi katika kukabiliana na maovu mengi na ukosefu wa haki unaotokea katika miji yetu mingi leo? Je, tunapaswa kuelewaje jukumu letu la Kikristo katika uhusiano na miji leo – je jukumu hilo limebadilika kutoka nyakati za manabii, na kama ndivyo, ni kwa jinsi gani? Kuulilia Mji Mkuu

3

3

Utume wa Kikristo na Jiji Sehemu ya 1: Kufafanua na Kutambua Uelewa wa Kibiblia wa Jiji

YALIYOMO

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Dhana ya mji inatawala ndani ya Agano la Kale na Agano Jipya, na inatupatia muhtasari rahisi wa sifa za miji ya kale. Miji katika ulimwengu wa kale ilikuwa tofauti na vijiji kwa kuwa ilikuwa ni mkusanyiko wa nyumba na majengo yaliyozungukwa na kuta, ilikuwa muhimu na yenye kuvutia kwa wakati wao, na

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook Annual report maker