https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 3 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

5. Inaonekana kwamba “miji na vijiji vyake” vilivyotajwa katika Maandiko vinaonyesha kwamba baadhi ya vijiji vilimilikiwa na miji na vilikuwa vinategemea miji (Yos. 13:23, 28; 15:32, 36, 41), na baadhi ya vijiji vilikua hadi kuwa miji kwa sababu ya idadi ya watu na umuhimu wake (k.m., Hasar-adari, Hes. 34:4; ambao uliunganisha Hesroni na Adari, Yosh. 15:3).

B. Sifa za miji ya kale

1. Kimsingi ilikuwa midogo, iliyojengwa na barabara za mitaa nyembamba, zilizopinda, ambapo masoko na mahakama zilikuwepo (Mhu. 12:4; Wim. 3:2; Mwa. 23:10; Ruthu 4:1).

2. Barabara chache sana ziliwekwa lami, ingawa Josephus anasema kwamba Sulemani alikuwa amejenga barabara za kuelekea Yerusalemu zilizowekwa lami (Antiquities of Josephus, 8:7).

3

3. Miji mikuu na miji muhimu iliimarishwa kwa kuta nene zenye ngome (2 Nya. 26:6; Sef. 1:16).

4. Minara mirefu iliinuliwa juu ya malango ya miji (2 Sam. 18:24; 2 Fal. 9:17 ); na kwenye pembe za kuta zenyewe (2 Nya. 14:7; 32:5).

5. Mifereji ilichimbwa na ngome kujengwa nje ya kuta, 2 Sam. 20:15; Isa. 26:1.

6. Majiji ni wazo la zamani: majiji kama vile Uru, Nippur, Kishi, Eridu, Lagashi, Ninawi, Ashuru na mengine yamechimbuliwa, huku wanaakiolojia wakikadiria kuwa miji hiyo ilikuwepo takriban miaka ya 3,000 K.W.K. na hata mapema zaidi ya hapo.

Made with FlippingBook Annual report maker