https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 3 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
II. Ufafanuzi wa Kibiblia: Kutambua Maana ya Kiroho ya Jiji
A. Mji unahusishwa na uasi wa binadamu na ibada ya sanamu: Kaini na mji wa Henoko.
1. Rekodi ya Biblia, Mwa. 4:16-17.
2. Kaini aliacha kutanga-tanga, akajenga mji, na kuupa jina la mwanawe (jina Henoko lina maan ya kuanzisha , au kuzindua , kwa maneno mengine, “mwanzo mpya”).
3. Wazo la mji halijaanzishwa na Mungu, bali ni wazo la yule aliyemuua ndugu yake na kisha kuujenga mji kuwa mahali pa kudumu na pa usalama .
3
B. Mji unahusishwa na uhuru na kiburi: Mnara wa Babeli, Mwa. 11:1-9.
1. Mji na mnara wake ulijengwa kwa kusudi la “tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote” Mwa. 11:4.
2. Madhumuni yenye pande mbili:
a. Tujifanyie jina : kuanzisha njia yetu wenyewe ya kuamua hatima na mafanikio yetu.
b. Tusipate kutawanyika : njia ya kuunganisha na kuimarisha nguvu iliyoratibiwa ya watu hawa huru na wenye kiburi.
3. Mnara wa Babeli ni ishara yenye nguvu ya jiji ya kukataa kabisa kumtegemea Mungu, na badala yake kutegemea kwa kiburi mipango na nguvu za kibinadamu.
Made with FlippingBook Annual report maker