https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 4 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
4. Safari za umisheni za Paulo kimsingi zilikuwa za mijini kabisa.
a. Huduma yake ilijumuisha kwenda katika miji mingi tofauti inayofunika eneo pana. (1) Mdo 20:23 (2) Rum. 15:19-23 b. “Kujishughulisha na miji haikuwa tabia ya Paulo peke yake.... ndani ya muongo mmoja wa kusulubishwa kwa Yesu, utamaduni wa kijiji cha Palestina ulikuwa umeachwa nyuma, na miji ya himaya ya Rumi yenye mchanganyiko wa kiutamaduni wa Kiyunani ikawa mazingira makuu ya harakati za Kikristo” (Wayne A. Meeks. The First Urban Christians: The Social World of the Apostle Paul. New Haven, CT: Yale University Press, 1983, uk. 9-11).
3
5. Kumtangaza Kristo na Ufalme wake (kiini cha utume) kulitokea katika maeneo ya mijini, katika miji, ambayo ilitumika kama lango la ufalme mkubwa wa Kirumi.
a. Matendo 8:5-6
b. Matendo 13:44
c. Matendo 14:20-22
d. Matendo 16:14
e. Matendo 18:8-10
Made with FlippingBook Annual report maker