https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 5 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
II. Jiji ni sumaku ya wanyonge, waliovunjika moyo na maskini
Mungu anapenda majiji kwa sababu huko ndiko hukaa mamilioni ya walengwa wa huruma yake. Jinsi jiji linavyoenda, ndivyo taifa linavyoenda, na ndivyo ulimwengu unavyoenda!
A. Moyo wa Mungu kwa maskini: agizo la kiroho.
1. Maandiko yanamfunua Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu kama Mungu anawayependa maskini na amewaita maskini, na miji ya ulimwengu imejaa umati wa watu ambao ni maskini, na dhaifu, na wanaodharauliwa.
2. Yesu alisema katika Luka 6 kwamba maskini, wale waliao na wenye njaa, wale waliochukiwa kwa ajili ya jina lake ndio waliobarikiwa kweli katika maisha haya.
3. 1Wakorintho 1:29 inasema Mungu alichagua wapumbavu ili kuwaaibisha wenye hekima, wanyonge ili kuwaaibisha wenye nguvu, na waliodharauliwa ili aaibishe walio na makuu.
3
4. Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa (Yak 1:27).
5. Zaburi 10:14 inasema kwamba Mungu ni msaidizi wa wanyonge, na kwamba anatenda haki kwa yatima na walioonewa, na mfungo wa kweli kulingana na Isaya 58 ni kuwaleta wasio na makazi na wenye njaa katikati yenu na kuwahudumia.
6. Yakobo 2:5 inasema kwamba Mungu amewachagua maskini wawe matajiri katika imani, na warithi wa Ufalme aliowaahidia wampendao.
B. Mwenendo wa maisha leo: ukuaji wa miji kama sifa yenye nguvu zaidi ya nyakati za sasa.
Made with FlippingBook Annual report maker