https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 5 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
1. Harvie Conn, “Utume Mjini.” Toward the 21st Century in Christian Mission. (Grand Rapids: Eerdmans, 1993). (Grand Rapids: Eerdmans, 1993). “Tunapoingia katika karne ya ishirini na moja mahitaji yataongezeka ... Dunia yetu itakuwa na miji mikubwa 433 yenye zaidi ya watu milioni 1 kila moja. Idadi ya watu mijini itaongezeka kwa watu milioni 1.6 kwa wiki. Umaskini katika maeneo yetu ya mijini utaendelea kuongezeka, na kutokeza “sayari ya makazi duni ya mijini.” Ili kukidhi mahitaji hayo, makanisa mapya lazima yapandwe kwa kasi kubwa. Kiwango cha upandaji makanisa katika miji ya ulimwengu bado hakiridhishi. Watu hawa wasioonekana, na wasiofikiwa wa majiji ya ulimwengu lazima wapatikane – maskini, wafanyakazi wa viwandani, wafanyakazi wa serikali, makundi mapya ya kikabila na ya kijamii wanaoishi katika maeneo ya mijini. Ikiwa tunataka kufikia ulimwengu wa karne ya ishirini na moja, lazima tufikie miji na majiji yake.”
2. David B. Barrett. “Jedwali la Takwimu la Mwaka juu ya Umisheni Ulimwenguni: 1999.” International Bulletin of Missionary Research . Toleo la 23, Nambari 1, Januari 1999.
3
a. Ifikapo mwaka wa 2025, idadai ya maskini wa mijini itakuwa zaidi ya watu bilioni 3 na hiyo itakuwa zaidi ya theluthi moja ya watu duniani. Zaidi ya watu bilioni mbili katika idadi hiyo watakuwa wamejazana katika makazi duni ya mijini.
b. Ulimwenguni pote leo, wakaaji wa mijini wasio Wakristo wanaongezeka kwa kasi ya watu 136,000 kwa siku. Idadi ambayo inakadiriwa kuongezeka hadi 360,000 kwa siku ifikapo 2025.
c. Mwaka wa 1900 tulikuwa na takriban watu milioni 100 maskini duniani. Karne moja baadaye idadi hiyo iliongezeka hadi watu maskini bilioni 1.92, na kufikia 2025 kutakuwa na zaidi ya watu bilioni 3 maskini duniani.
Made with FlippingBook Annual report maker