https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 5 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

3. Hoja ya kibiblia: ikiwa Mungu anawajali maskini, ni lazima pia anajishughulisha sana na majiji ya Marekani na kote duniani!

a. Umaskini nchini Marekani unaendelea kuongezeka; taarifa za hivi punde zaidi zinazopatikana kutoka Ofisi ya Sensa ya Marekani kwa mwaka wa 2001, zinaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watu walio katika umaskini nchini Marekani hadi kufikia milioni 32.9, jambo ambalo linaweza pia kuakisi ongezeko la takwimu za umaskini katika maeneo ya majiji. Kwa mara ya kwanza katika takriban muongo mmoja, umaskini nchini Marekani uliongezeka mwaka jana, huku mapato ya wastani yakishuka. Kulingana na Ofisi ya Sensa, viashiria vyote hasi vya kiuchumi viliambatana na mdororo wa uchumi. Kiwango cha umaskini kilipanda hadi asilimia 11.7 mwaka 2001, kutoka asilimia 11.3 mwaka 2000. Lilikuwa ni ongezeko kubwa la kwanza la umaskini mwaka hadi mwaka tangu 1991 - 92. Wakati huo huo, mapato ya wastani ya kaya yalipungua kwa asilimia 2.2 kwa jumla kutoka kiwango chake cha mwaka 2000 hadi kufikia Dola 42,288 za Marekani.

3

b. Idadi ya maskini inaendelea kuongezeka; Ripoti ya Sensa inaonyesha kwamba watu milioni 1.3 zaidi walikuwa maskini mwaka 2001 kuliko mwaka 2000 – milioni 32.9 ikilinganishwa na milioni 31.6.

C. Ikiwa umisheni unahusu miji na majiji, basi utalazimika pia kuwahusu maskini, kwa sababu idadi kubwa ya watu mjini ni maskini.

1. Mungu alihukumu watu wake kwa sababu ya uasherati wa miji yao na ukandamizaji wa maskini wao, Amosi 2:6-8.

2. Ongezeko la idadi ya watu kwa mamilioni huko nje ya nchi na kuongezeka kwa idadi ya watu hapa nyumbani kunaonyesha kuwa miji yetu ni sumaku inayowavuta watu maskini zaidi katika ulimwengu wetu wa leo.

Made with FlippingBook Annual report maker