https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 6 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
7. Biblia inafunuaje “ushahidi ulio wazi na wenye nguvu” kuhusu moyo wa Mungu kwa maskini? Ikiwa ni kweli kwamba Mungu anajali sana maskini, kwa nini basi pengine tunaweza kusema kwamba anajishughulisha pia na majiji ya Marekani, na miji mikubwa ya ulimwengu? 8. Ni katika maana gani ukweli kuhusu Yerusalemu Mpya unadhihirisha chaguo la Mungu la jiji kuwa picha na ishara ya hatima na urithi wetu wa kiroho? Je! Yerusalemu Mpya inatofautianaje na maana ya majiji ya kiulimwengu yanayoakisiwa kupitia majiji makubwa ya wakati uliopita? 9. Ni nini lengo lililo wazi la utume katika mtazamo wa uhusiano kati ya majiji ya ulimwengu huu uliopotea na makao ya wenye haki, Yerusalemu Mpya? 10. Hatimaye, kwa nini ni lazima kila mara tuweke huduma na umisheni wa mijini kuwa kipaumble cha maombi yetu yote, utoaji wetu, kwenda na kuwatuma wengine kuhudumu mjini? Kulingana na Neno la Bwana mwenyewe, ni jinsi gani tunaweza kuhakikisha ustawi wetu tunapokaa katikati ya jamii za mijini zenye shida na uhitaji mwingi? Utume wa Kanisa unaweza kujumlishwa katika kazi tano za jumla. Mpangilio ambao zimeorodheshwa hapa chini haukusudiwi kuonyesha vipaumbele katika umuhimu wake. Kuzungumza kibiblia, kila kipengele hapa ni cha muhimu sana. Kwa kukazia kipengle kimoja zaidi kuliko nyingine, vikundi mbalimbali vya Wakristo vimeelekea kuona baadhi ya vipengele hapa kama mambo ya ziada. Hata hivyo, Mungu haruhusu hilo! 1. Ni kuhusika katika kusimamia rasilimali za uumbaji . Hii ina maana ya kuhimiza matumizi yenye hekima na uwiano ya uumbaji wa asili wa Mungu, kwa kujihusisha katika vipengele vingi vya uhifadhi na kutokomeza uchafuzi wa mazingira. Kanisa litaelekeza watu kwenye kuheshimu na kuthamini zawadi ya Muumba ya uhai kwa wote ambayo ina maana ya kupinga uchoyo na ubinafsi, na kuhimiza kuwa na kiasi katika matumizi ya rasilimali kwa wote kwa njia ambayo vizazi vijavyo vitaweza kuishi maisha yenye ustawi endelevu duniani. 2. Ni kuwahudumia wanadamu bila ubaguzi na kwa mahitaji yao yoyote . Kanisa lina kazi ya huruma ya kuwasaidia wakimbizi na wahanga wa ukame na njaa na kusaidia kuanzisha miradi ya maendeleo, kampeni za kusoma na kuandika, elimu ya afya na programu za makazi. Lina jukumu Kwa Kuzingatia Uhitaji wa Jiji, Utume wa Kanisa ni Nini?
3
Made with FlippingBook Annual report maker