https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 6 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kufanya marudio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video. Katika sehemu hii tulizingatia sababu tatu za umuhimu wa miji katika umisheni ndani ya karne ya 21. Kwanza, miji ni makao ya ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho katika ulimwengu wa leo; kupitia ukuaji wa miji na uhamiaji, miji pia inakuwa sumaku kwa watu waliokandamizwa, waliovunjika moyo na maskini duniani. Hatimaye, Maandiko yanaweka wazi kwamba jiji ndilo picha na ishara ya uhakika na ya mwisho ya hatima na urithi wetu wa kiroho. Sababu hizi zinaleta mantiki ya wazi kwa ajili ya ufikiaji makini na wa kimkakati kwa miji ya dunia. Fanya marudio ya mawazo makuu yanayohusiana na sababu hizi kupitia maswali yaliyo hapa chini. 1. Orodhesha sababu tatu zinazoonyesha kwa nini umisheni wa mijini lazima uwe kipaumbele kwa shughuli zote za umisheni leo. Kati ya hizo tatu, ni ipi ambayo unaamini kuwa ndiyo sababu kuu? Elezea jibu lako. 2. Jiji lilikuwa na sehemu gani katika huduma ya Yesu na mitume? Yerusalemu ilikuwa na nafasi gani katika kazi yao ya kuendeleza Ufalme? Je, ni kwa jinsi gani ujumbe wa Kikristo ulienea katika milki ya Kirumi, na ni jinsi gani jambo hili lilionyeshwa hasa katika safari za Paulo? 3. Vituo vikubwa vifuatavyo vya ufalme wa Kirumi vilikuwa na uhumimu gani katika kuendeleza Injili katika Kanisa la kwanza (k.m., Dameski, Antiokia, Korintho, Filipi, Thesalonike, Athene, na Roma yenyewe)? 4. Matatizo yaliyopatikana katika miji ya kale yanalinganishwaje na fursa na matatizo tunayopata leo katika majiji ya kisasa? Majiji ya leo yanatofautianaje kwa ukubwa, upeo, ushawishi, na idadi ya watu? Ni katika maana gani tunaweza kusema kwamba majiji ya kisasa “yanatumika kama vitovu vya kitaifa na vya ulimwengu vya serikali, elimu, afya, habari, burudani, biashara, viwanda, sheria, jeshi, na dini”? 5. Orodhesha aina mbalimbali ambazo wanaanthropolojia hutumia leo kutambua miji. Orodhesha sifa za aina zifuatazo, pamoja na ufafanuzi na mifano ya kila moja: miji ya kitamaduni , miji ya kisiasa na kiutawala , miji ya viwanda , miji ya kibiashara , miji ya alama au ya kihistoria na miji ya msingi . 6. Katika ulimwengu wa sasa ni nini kinachosababisha idadi kubwa namna hii ya waliokandamizwa, waliovunjika moyo, na maskini kuhamia maeneo ya mijini? Ni katika maana gani tunaweza kusema kwamba kukua kwa miji kunawakilisha “sifa yenye nguvu zaidi ya nyakati za sasa?”
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
3
Made with FlippingBook Annual report maker