https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 6 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
IV. Dondoo za mwisho kwa ajili ya huduma mjini
A. Katika shughuli zetu zote za umisheni: kuomba, kutoa, na kutuma watu, lazima tuzingatie miji.
1. Kwa sababu ya umuhimu wake wa kimkakati.
2. Kwa sababu ya umuhimu wake wa kimishenari.
3. Kwa sababu ya umuhimu wake wa kiroho.
B. Tuwe na fahari na shukrani kwa sababu ya wajibu wetu wa kumwakilisha Bwana mjini.
3
C. Tuwe na mikakati na ubunifu wa jinsi tunavyoweza kuathiri maeneo mengi kupitia mbinu ya kujenga mahusiano na mawasiliano na kizazi cha kwanza katika wana-familia wa karibu ili kufikia mitandao mipana zaidi ya watu wanaohusiana nao ( oikos, oikia ).
D. Ombea miji, na utafute afya na ustawi wake, kwani katika usalama wake uko usalama wetu, Yer. 29:4-7.
Hitimisho
» Kuna sababu tatu zenye nguvu na ushawishi za ushiriki wa Kanisa katika utume wa mijini. » Miji ni makao ya ulimwengu ya ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho, ni sumaku kwa waliokandamizwa, waliovunjika moyo, na maskini. Ni picha kuu na ishara ya hatima na urithi wetu wa kiroho.
Made with FlippingBook Annual report maker