https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 5 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
2. Yesu ndiye Mkandarasi wa Ulimwengu, ambaye kwa mpango na uwezo wake mwenyewe anatutengenezea jiji la kuishi. Maisha ya mwanadamu yalianza katika bustani, lakini yataisha, hatimaye, katika mji wa Mungu uliojengwa na Bwana wetu, Yohana 14:1-4.
3. Utambulisho na uraia wetu wa kweli unahusishwa na mji huu wa Mungu, Flp. 3:20-21.
C. Lengo la wazi la utume (uinjilisti, kufuasa na upandaji makanisa) ni kuvuna miji iliyopotea ili kujaza vitabu vya Yerusalemu Mpya, ambayo ni mama wa kweli wa waamini wote.
1. Yerusalemu ya juu ndiye mama yetu wa kweli, Gal. 4:26.
3
2. Orodha ya majina iliyopo juu ndiyo ya maana zaidi kwetu kupatikana ndani yake, Zab. 87:3-6.
3. Neno la Bwana litatoka Yerusalemu.
a. Isaya 2:2-3
b. Marko 4:1-2
4. Furaha na shangwe hazitaondoka katika mazingira yake, Isa. 65:18.
5. Mungu mwenyewe atakaa pamoja na watu wake katika mradi wa mwisho wa ukarabati wa miji, Yoeli 3:17.
Made with FlippingBook Annual report maker