https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 6 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
na majiji ya Marekani na dunia kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wa tabaka la chini na familia maskini zinazoishi kwa kujazana humo. ³ Biblia inaonyesha wazi jinsi mji ulivyo picha na ishara ya hatima na urithi wetu wa kiroho. Tumaini la watakatifu ni kukaa na Mungu katika Yerusalemu Mpya, si mahali ambapo Mungu hayupo na ambapo majivuno yanatawala, bali ni nyumba ya wenye haki ambapo Mungu yupo, na Yesu anaabudiwa kama Bwana wa wote. ³ Lengo la wazi la utume ni kuvuna miji ya dunia ili kujaza Yerusalemu Mpya, mama wa kweli wa waamini wote (mradi wa mwisho wa ukarabati wa miji). ³ Kwa sababu ya umuhimu wa mji katika Maandiko na katika ulimwengu wa sasa, mji lazima ubaki kuwa kitovu cha shughuli zote za kimishenari. Kuomba kwetu, kutoa, na kutuma watenda kazi lazima kulenge kufikia miji ambayo haijafikiwa, lazima tuajiri wamishenari zaidi kuhudumu katika mji, kupanga mikakati ya jinsi ya kufikia miji ambayo haijafikiwa na Injili, na kuombea miji na kutafuta usalama wake, yaani kutafuta usalama wetu katika uhifadhi wake. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu jiji na nafasi yake katika umisheni leo. Hapa kuna fursa ya kujadili mawazo yako kuhusu jiji, na masuali maalum uliyo nayo kuhusu umisheni na jiji kwa kuzingatia yale uliyojifunza hivi punde. Kipaumbele hapa ni juu ya maswali yako; tumia maswali yaliyopo hapa chini kuunda orodha yako mwenyewe ya masuala na maswali. * Je, una maoni gani kuhusu mji—ulikulia wapi, na familia yako na watu walioishi katika jamii yako waliuonaje mji huo? Je, ungeweza kuelezeaje hisia zako kuhusu mji huo leo? * Je, ni rahisi kwako kuona uhusiano kati ya uasi wa kibinadamu, ibada ya sanamu, uhuru, na kiburi na miji ya kisasa ya Marekani na kwingineko duniani? Je, unafikiri kwamba Mungu atahukumu miji ya kisasa ya Marekani kama alivyohukumu miji ya kale kwa sababu ya dhambi na ugumu wa mioyo yao? Eleza. * Je, unahusisha jiji lolote na maana ambayo tumegundua katika somo letu leo, yaani, kama ishara ya makao ya Mungu na baraka zake? Je, hili linaweza kusemwa tu kuhusu Yerusalemu Mpya, au je, tunapaswa kujitahidi kuona miji yetu leo kwa njia hii? Eleza.
3
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
Made with FlippingBook Annual report maker