https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 6 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

* Ikiwa ungeweza kuishi katika jiji lolote nchini, lingekuwa lipi na kwa nini? Je, una “maeneo ya upofu” yoyote kwa sasa kuhusu jiji, kwa maneno mengine, je, unashindwa kuona mambo kwa usahihi (yawe mazuri au mabaya) kuhusiana na miji kwa sababu ya upendeleo wako ama kwa kutopenda kwako miji? * Je, unaweza kufikiria kufanya umisheni mijini, kupanda makanisa na kufanya wanafunzi katika jamii za mijini? Vipi kuhusu jamii za watu masikini wa mjini – je, kwa sasa una mtazamo wowote hasi kuhusiana na kufanya huduma mjini? * Kwa kawaida unawaonaje watu katika miji na majiji—je, wao ni wahasiriwa wa ukandamizaji, au unadhani chochote kibaya wanachopitia ni haki yao na matokeo ya matendo yao wenyewe na uzembe wao? Eleza jibu lako. * Unafikiri ni kwa nini Wakristo wachache sana Marekani wanaonekana kuwa na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa idadi ya watu wa hali ya chini mijini ambao hawapati huduma za Kanisa katika tamaduni na lugha zao wenyewe? Kwa nini wengi hulaumu hali za wakazi wengi wa mijini wanaoteseka wakiwashutumu kwamba ni kwa sababu ya ukosefu wao wa uadilifu na kutowajibika kibinafsi? * Kamilisha sentensi ifuatayo: “Kabla sijahisi amani na uhuru wa kwenda na kufanya umisheni mjini, Bwana ingenibidi . . . * Je, unatamani Mungu ahukumu baadhi ya majiji yaliyopo leo? Elezea. Unafikiri kwamba ikiwa majiji ya kisasa yangetubu na kujinyenyekeza mbele za Bwana kama walivyofanya Waninawi, Mungu anaweza kuitikia kwa namna ileile na kuwasamehe? * Wengi huyatazama majiji kama mahali tu pa kutembelea likizo au wakati wa mapumziko. Je, unaweza kusema nini kwa sasa kuhusu uhusiano wako na miji, na watu wanaoishi humo—una wajibu na mzigo gani binafsi kuhusu jiji, na wito wako wa kuhudumu mjini? * Je, unaomba kwa ajili ya miji ya ulimwengu? Ikiwa sivyo, kwa nini? Je, unaombea jiji lako mwenyewe, viongozi na watawala wake, idadi ya watu na mahitaji yake, fursa zake, na njaa ya kiroho? Unawezaje kuanza kuomba kwa umakini zaidi kwa niaba ya wale wanaoishi katika jamii yako ya mjini? Je, unatoa na kuunga mkono umisheni wa mijini ndani ya nchi? Ulimwenguni kote? Wapi? (Ona “Acha Mungu Ainuke” katika viambatisho vya moduli hii).

3

Made with FlippingBook Annual report maker