https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 6 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
* Je, inakufurahisha kwamba Yesu anatujengea jiji la kukaa milele? Kuwa mkweli iwezekanavyo katika majibu yako. Je, unauelewa umisheni kama kazi ya kuvuna miji ya ulimwengu ili kujaza Yerusalemu Mpya, mama wa kweli wa waamini wote?
MIFANO
Kuwa Kasisi au Kufanya Suluhu?
Dhana ya Kanisa kama kasisi wa jiji imejikita katika maagizo ya Bwana kupitia Yeremia kwa watu wa Yuda kabla ya utumwa wao Babeli. Badala ya kuwafanya wavunjike moyo na kukata tamaa wakiwa Babiloni, Mungu aliwaagiza kulea familia zao ndani yake, na kutafuta ustawi wake: “ Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, awaambia hivi watu wote waliochukuliwa mateka, niliowafanya wachukuliwe toka Yerusalemu mpaka Babeli; 5 Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake; 6 oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue. 7 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani ” (Yer. 29:4-7). Kisa hiki cha utumwa wa Babeli kinazua maswali kuhusu msimamo ambao waamini wanapaswa kuchukua kuhusu jiji lenye uovu na lisilomcha Mungu. Badala ya kulipinga na kuzua matatizo ndani yake, Mungu anaagiza kwamba watu wake wajenge familia zao katikati ya jiji hilo, walee familia zao humo, na hata waongezeke na kukua humo. Amri ya kutafuta ustawi wa jiji hilo inaonekana kuwa na utata; ni jinsi gani ustawi wa watu wa Mungu unaweza kuunganishwa moja kwa moja na usalama na ustawi wa Babeli, ambayo ni ishara ya ibada ya sanamu na uasi mbele za Mungu? Maagizo ya Mungu kwa Waisraeli yanatuambia nini kuhusu nafasi ya watu wa Mungu kwa jiji hilo, na ni mambo gani tunayoweza kujifunza kutokana na hilo kwa faida yetu leo? Kanisa kubwa la mjini na linalokua la Wamarekani Weusi linatatizika kuamua iwapo litakaa katika eneo lilipo sasa, au kuhamia sehemu inayoendelea na yenye hali ya juu zaidi ya mji. Likiwa na mchungaji mwenye nguvu ambaye amejitoa kwa dhati katika Neno na maendeleo ya Ufalme, kanisa limeendelea kukua katika idadi, ushawishi, na rasilimali. Wakiwa na akiba kubwa ya viongozi wenye uwezo na utii, na kusanyiko lililo na shauku ya kutumikia, viongozi wanafikiria kwa uzito ikiwa wanapaswa kuhama. Hawawezi kujenga majengo na miundo-mbinu mingine mikubwa zaidi, bora na ya kisasa kwa sababu ya ufinyu wa eneo lao la sasa. Wana huduma kadha wa kadha katika jamii ambazo zinalenga wana-jamii walio Kubaki Hapo Hapo au Kusonga Juu na Nje?
1
3
2
Made with FlippingBook Annual report maker