https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 6 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
na uhitaji zaidi; kanisa limekuwa katika eneo hilo kwa miongo kadhaa, na sasa liko katikati ya maboresho makubwa. Kwa kuwa mchungaji wao anazidi kuwa mtu mwenye ushawishi katika jiji na nchi nzima, viongozi wanashawishika kwamba kwa kuhama na kujenga katika eneo lingine, wanaweza kuongeza sana fursa zao za huduma na mguso kwa jiji. Wengine, wanaoliona kanisa kuwa chumvi na nuru ya mtaa wao wa sasa wenye umaskini katika jiji hilo, wanashindana na wazo la kanisa kuondoka mahali ambapo pana uhitaji mkubwa na kuhamia katika jamii ambayo ni tajiri na “salama.” Ikiwa ungeitwa kumshauri mchungaji na viongozi juu ya uamuzi wao ujao, ni kanuni na mitazamo gani ungewapa kuhusu mwelekeo unaofikiri wanapaswa kuchukua? Mzozo umezuka katika kanisa la mjini ambalo hivi majuzi lilianzisha mfululizo wa huduma za uinjilisti katika sehemu maskini sana na iliyojitenga ya jiji kubwa la Magharibi Kati. Akiwa amechochewa na shauku kubwa ya kwenda mahali ambapo makanisa na huduma nyingine hazikuwa tayari au ziliogopa kwenda, mchungaji alifundisha na kuagiza timu ya ushuhudiaji kwenda katika majengo ya ghorofa ya wapangaji katika eneo hilo kuhubiri Injili. Mapokezi ya wakazi wengi wa eneo hilo la maghorofani yalikuwa ya kushangaza, ikiwa ni pamoja na hata wasimamizi wa jengo hilo, ambao waliruhusu timu hiyo kutumia vyumba kadhaa vilivyokuwa wazi bila wapangaji. Kwa kuona kiasi kile cha kutosha cha kuvutiwa na ushiriki, haikuchukua muda mrefu kabla ya timu kuanzisha darasa la kujifunza Biblia mahali hapo, na kuona matunda – baadhi ya familia na watu binafsi waliohudhuria walimpokea Kristo. Wakati wa moja ya vipindi vya jioni, mgeni mmoja aliyealikwa na mkazi wa nyumba hiyo alielezea hisia zake kuhusu timu hiyo ya ushuhudiaji na kanisa lililowatuma. «Siwajui ninyi watu, na kwa kweli mnaonekana ni watu wazuri. Lakini, sielewi jinsi mnavyoweza kusema kwamba Mungu amewatuma humu ndani kutushirikisha Habari Njema ‘kuhusu Yesu,’ lakini hakuna kilichobadilika katika mtaa wetu. Magenge bado yanaendelea na wazimu wao, hakuna ajira popote, na wengi wetu tunahangaika ili kuishi. Aina hiyo ya Habari Njema haitii moyo – hakuna kinachobadilika hapa!» Ungejibuje uchambuzi na mashaka ya huyu dada mpendwa? 3 Aina Hiyo ya Habari Njema Haitii Moyo – Hakuna Kinachobadilika Hapa!
3
Made with FlippingBook Annual report maker