https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 7 0 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Njama ya Kiinjili dhidi ya Jiji la Marekani?

(Inatokana na kisa cha kweli). Chuo maarufu cha uzamili cha Kikristo kilikuwa kikianzisha na kufadhili mipango kadhaa ili kufikia watu ambao hawajafikiwa kote ulimwenguni, wakiwemo Waislamu, Wachina na Waslavoni. Masomo mengi yalitolewa kwa wanafunzi wa kimataifa walio na mzigo wa huduma, na shule imeandaa mamia ya watenda kazi wa kiroho waliohitimu wanaomtumikia Kristo katika maeneo mbalimbali kote ulimwenguni. Hata hivyo, umbali wa chini ya dakika 25 kutoka chuo hicho, kulikuwa na mojawapo ya mitaa duni mikubwa zaidi nchini Marekani. Zaidi ya watu milioni moja wanaishi katika makazi duni katika vitongoji vyenye jeuri, magenge na dawa za kulevya, na kwa hakika hakuna vikundi vya Kikristo vinavyohudumu katikati yao. Alipokabiliwa na maswali magumu kuhusu tofauti katika uwekezaji wa chuo wa maelfu ya dola na nguvu kazi katika umisheni wa nje ya nchi wakati hakuna chochote ambacho chuo kinafanya kwa ajili ya kuzifikia jamii zenye uhitaji katika maeneo ya jirani ya ndani ya nchi, mkurugenzi wa chuo hicho alisikitika na kuelezea jinsi ilivyokuwa ngumu kupata wafadhili wa kufadhili mipango ya kufikia watu miongoni mwa maskini wa miji ya Marekani. Aliona ni rahisi kuchangisha pesa kwa ajili ya mafunzo ya watu nchini Honduras kuliko jijini Houston, nchini Jamaika badala ya Jiji la Jersey. Je, unaweza kuelezea vipi hali hii ya kutojali kwa jumla kwa waumini wa makanisa ya kiinjili kuhusu mahitaji na fursa za utume katika majiji? Kwa nini iwe rahisi kwa mkurugenzi wa chuo kuchangisha fedha nyingi kwa ajili ya huduma nje ya nchi, na bado anaona ni vigumu kuwashawishi watu kufadhili mafunzo ya watenda kazi kwa ajili ya miji ya Marekani? Dhana ya mji inatawala ndani ya Agano la Kale na Agano Jipya, na inatupatia muhtasari rahisi wa sifa za miji ya kale. Miji katika ulimwengu wa kale ilikuwa tofauti na vijiji kwa kuwa ilikuwa ni mkusanyiko wa nyumba na majengo yaliyozungukwa na kuta, ilikuwa muhimu na yenye kuvutia kwa wakati wao, na baadhi ya miji ilitegemea miji mingine kwa ajili ya ulinzi na mahitaji muhimu. Ukweli wa kawaida katika ulimwengu wa kale, miji ya zamani ilikuwa midogo, kwa kawaida isiyo na lami, iliyoimarishwa kwa kuta nene na minara mirefu, na vituo vya serikali na mamlaka. Kuhusu maana yake ya kiroho kama ilivyoainishwa katika Maandiko, miji ilihusishwa na uasi wa kibinadamu na ibada ya sanamu (k.m., Henoko, jiji la Kaini), na uhuru na kiburi (kama ilivyokuwa kwenye Mnara wa Babeli), na uovu na kutomcha Mungu (kama vile Babeli). Miji ilihukumiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi yake (k.m., Sodoma na Gomora, Yeriko, Ninawi), na kushutumiwa kwa kujidhania kwa uongo kwamba ina usalama na uwezo (hasa, Yerusalemu). Ingawa Maandiko yanahusianisha mji wa Yerusalemu na uasi wa

4

3

Marudio ya Tasnifu ya Somo

Made with FlippingBook Annual report maker