https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 7 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Utume wa Kikristo na Maskini
SOMO LA 4
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kufafanua dhana ya maskini katika mwanga wa maono ya kibiblia ya shalom, au ukamilifu: shalom ni neno la Kiebrania linalomaanisha “ukamilifu wa jamii ya wanadamu katika ushirika na Mungu na baina yao mmoja kwa mwingine.” • Kuelezea vipengele vya shalom ikijumuisha uzima na afya njema, usalama na ulinzi, maelewano kati ya majirani, ustawi na utoshelevu wa mali, na kukosekana kwa uovu na migogoro – Amani ya kweli na kamilifu. Hili pia linajumuisha wazo la shalom kama utoaji wa Mungu kwa msingi wa neema yake, unaohusishwa na ujio wa Masihi ambaye ni Mfalme wa shalom , pamoja na shalom kama kiwango cha maisha kwa watu wa Mungu. • Kueleza jinsi ambavyo umaskini ni kunyimwa shalom ya Mungu, jinsi baraka yake ilivyokusudiwa kuzuia kutokea kwa umaskini, na namna Mungu alivyotoa amri na maagizo kwa jamii ya agano ili kuhakikisha uwepo wa haki na uadilifu kati ya watu wa Yehova, na kwamba uaminifu kwa agano ulikusudiwa kwa ajili ya kuendeleza shalom kati ya Waisraeli kwa sababu ya kule kutii sauti yake na kutimiza masharti yake. • Kuonyesha jinsi Mungu anavyohusishwa na watu maskini, yaani, ni mpango wake kuwainua na kuwabariki kutoka katika hali yao, kuwaadhibu wale wanaowadhulumu, na kuwataka watu wake waonyeshe hali ya kujali ile ile aliyo nayo kwa niaba ya waliovunjika moyo, maskini, na waliokandamizwa. Tukio la “Kutoka” ni tukio muhimu ambalo linajumuisha utambulisho wa Mungu na watu maskini na walioonewa, likifunua moyo wake wa haki na kuundwa kwa jamii yake ya agano ambayo iliitwa kuwa kielelezo cha utakatifu wake, taswira ya haki na rehema zake, na nuru kwa mataifa. • Kuweka wazi sababu za kibiblia za umaskini, ikiwa ni pamoja na majanga ya asili na maafa (k.m., njaa, ukame, vimbunga, n.k.), uzembe na uvivu wa mtu binafsi (k.m., maamuzi mabaya, tabia mbaya, uvivu, mioyo migumu, n.k.), na ukandamizaji na ukosefu wa haki unaosababishwa na watu wenye nguvu na mamlaka (k.m., unyanyasaji, unyonyaji, dhuluma ya malipo na haki za wengine). Neno “maskini” katika Maandiko linahusianishwa
Malengo ya Somo
4
Made with FlippingBook Annual report maker