https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 7 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
na dhana mbalimbali zinazotumika kama visawe, kutia ndani “mjane,” “yatima,” na “mgeni.” • Kuorodhesha viwango au maagizo ambayo Mungu aliwapa watu wake wa agano kuhusiana na namna ya kuwatendea maskini kwa ukarimu na haki. Haya yanahusisha masharti maalum ya kuwatunza maskini ambayo yaliwekwa katika maagizo ya Sheria (Torati) kuhusiana na mavuno na masazo yake, haki katika mahakama ambapo mambo yote, hatua zote, na shughuli zote zilipaswa kufanyika kwa uaminifu na kwa haki, bila kujali hali ya mtu; na rasilimali zilipaswa kugawanywa katika mwaka wa Sabato, na maskini walipewa sehemu ya mazao ya mashamba na mizabibu. • Kuorodhesha zaidi maagizo hayo, ikijumuisha jinsi watu wa Mungu walivyokatazwa kutoza riba kwa maskini, walivyoagizwa kutoa malipo ya haki na kwa wakati kwa kazi ya siku moja (yaani, mishahara au posho kulipwa siku hiyo hiyo bila dhuluma au ulaghai wowote), pamoja na kuwatendea maskini kwa ukarimu wa kiwango cha juu (“sera ya mkono wazi”), na kutenga rasilimali kwa ajili yao (sehemu ya zaka na fadhila kutolewa kwa wahitaji na watu walio hatarini zaidi katikati ya jamii). Maskini walipaswa kujumuishwa katika sherehe na siku kuu zote, na katika mwaka wa Yubile, maskini walipaswa kurejesha (kukomboa) mashamba yao na mali zao, pamoja na wale ambao hawakuwa na fedha za kutosha kukomboa mali zao. • Kuelezea maana ya maagizo au viwango hivi kwa jamii ya agano la Mungu: katika shughuli zao zote, Watu wa Mungu walipaswa kuakisi moyo wa Mungu kwa maskini, kwa msingi wa ukombozi wa Mungu kwao katika “Kutoka”, na walipaswa kuonyesha shalom ya Bwana katika mahusiano yao yote na kushughulika kwao na watu wengine. • Kuthibitisha kwamba Kanisa ambalo Yesu alilianzisha ni jamii ya ufalme ya agano jipya la Mungu, iliyoitwa kuonyesha shalom ile ile katikati ya watu wa Mungu. • Kuelezea jinsi umasihi wa Yesu ulivyozinduliwa kupitia matendo ya uponyaji kwa walioonewa na kuhubiri Habari Njema kwa maskini (ambao walikuwa walengwa wa upendo wake, wito wake, huduma yake, na kusudi lake). Kadhalika, utaweza kuelezea jinsi Yohana Mbatizaji alivyothibitisha umasihi wa Yesu kupitia matendo ya haki na kuwahubiria maskini. Zaidi ya hayo, utaweza kuonyesha jinsi Yesu alivyohakiki na kuthibitisha wokovu wa watu kwa kuzingatia namna walivyowatendea maskini, na jinsi alivyojihusisha kikamilifu na “walio wadogo” (yaani, wenye njaa, wenye kiu, wageni, walio uchi, wagonjwa, na wafungwa).
4
Made with FlippingBook Annual report maker